BAVICHA wapewa mbinu ya ushindi 2020.soma zaid.
Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Dkt Vicent Mashinji amewataka
vijana wa Bavicha kutokuwa wazembe
wakufikiria bali kujipanga kwa ajili ya kushika
dola mwaka wa uchaguzi mkuu 2020 huku
akiwapatia kanuni za kushinda uchaguzi huo.
Akizungumza na vijana hao jana jijini Dar es
salaam Mashinji aliwaambia vijana hao chama
chao kimejipanga kushika dola hivyo wao kama
vijana wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza
majukumu ya kufanya uchaguzi na kuwatambua
wanachama hai, pia kuhakikisha kuwa uchaguzi
wa serikali za mitaa vijana wanashiriki nafasi
mbali mbali na kushinda
”Nataka niwape majukumu matatu ambayo
mkiyafanya hayo 2020 tutashinda nakutangazwa,
moja hakikisheni tunaingiza wanachama wapya na
kuwahakiki walio hai, nendeni 2019 kwenye
serikali za mitaa vijana mgombee na tupate
viongozi ngazi ya chini viijana wasomi, na tatu
kwa mwaka huu kila kijana ajue nafasi
zitakozogombewa katika eneo lake hiyo itatusaidia
kushinda nafasi nyingi za madiwani kwa
Tanzania bara na visiwani na haya ndiyo
majukumu makubwa ninayowapatia” Alisema
Mashinji.
Pamoja na hayo aliwataka vijana hao kuendelea
kupigania haki za wanyonge na kushinda vita ya
demokrasia bila kuvunja sheria huku akiwaasa
kuwa askari mzuri na shujaa ni yule
anayepambana bila risasi.
”Askari mzuri ni yule ashindaye vita bila kutumia
risasi zake, mkawe mabalozi wa kuwatetea
wanyonge na haki zao, msiwe waoga kudai katiba
ya wananchi, pia kuna watu Geita, Shinyanga na
Simiyu tunataarifa wanapigwa kisa itikadi ya
upinzani wa vyama hivyo kama vijana mnatakiwa
mpaze sauti kwa ajili yao”. aliwaambia Mashinji.
Hata hivyo Mashinji aliwaasa vijana hao kuwa
wapole na kusubiri maamuzi ya viongozi wa
chama kwani yanabusara. Aidha aliwapongeza
vijana hao kwa kuwa na umoja wa kupigania
haki na misingi ya demokrasia.
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Patrobas Katambi
alimweleza Katibu huyo wa chama kuwa wao
wapo tayari kwa pambano japo wanasikiliza na
kutii kauli ya chama hivyo wao watatoa
msimamo wao.
”Sisi vijana tupo tayari miili yetu ilale makaburini
na tukumbukwe kama mashujaa waliokufa
wakipigania haki, tumesikiliza maagizo ya viongozi
wetu lakini pia sisi leo tutatoa msimamo wetu”.-
Katambi
0 comments :
Post a Comment