Hii ni Rasimi# Poul Pogba amesaini kujiunga na manchester united miaka mitano.soma zaid.
WAZUNGU wanasema kwa Kiingereza chao, Deal
done. Yaani biashara imekwishamalizika. Watu
wananyanyuka katika viti vyao, wanapeana
mikono, wanakumbatiana, wanaondoka.
Uhamisho wa Paul Pogba inasemekana
umemalizika.
Manchester United imefanikiwa kumnasa kiungo
huyo mahiri wa Juventus kwa dau la Pauni 100
milioni ambalo litaweka rekodi mpya ya uhamisho
duniani na kulipiku dau la Pauni 85 milioni
ambalo Real Madrid walilipa mwaka 2013
kumchukua Gareth Bale kutoka Tottenham.
Licha ya kulipa dau hilo, United watamlipa Pogba
mshahara wa pauni 210,000 kwa wiki kwa
mkataba wa miaka mitano ikiwa ni miaka minne
tangu alipomruhusu kuondoka bure kwenda
Juventus Julai 2012 akiwa mchezaji kinda.
Bosi wa Man United, Ed Woodward alikacha
kwenda katika ziara ya United nchini China na
alikutana na Wakurugenzi wa Juventus, Giuseppe
Marotta na Fabio Paratici, pamoja na wakala wa
Pogba, Mino Raiola kwa ajili ya kumaliza dili hilo.
Juventus iling’ang’ania dau hilo licha ya Man
United kujaribu kushusha, lakini mwishowe Man
United imekubali kulipa dau hilo kwa staa huyo
mwenye umri wa miaka 23 ambaye amezaliwa
nchini Ufaransa na wazazi wake waliotokea
Guinea barani Afrika.
Kocha wa Man United, Jose Mourinho alikuwa
anamtaka staa huyo kabla ya pambano la ngao la
hisani kati yao na Leicester City Agosti 7 na
atajiunga nao mara baada ya timu hiyo kurejea
katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini
China ambako wametua juzi.
Pogba aliondoka Old Trafford katika utawala wa
kocha mkongwe, Sir Alex Ferguson baada
kushindwa kuhakikishiwa nafasi katika kikosi cha
kwanza kilichokuwa kimesheheni mastaa
wakongwe kama Paul Scholes ambaye Ferguson
hakutaka kumuweka benchi na alimuamini zaidi.
Tangu hapo, Pogba ameibuka kuwa mmoja kati
ya viungo bora barani Ulaya huku akiiwezesha
Juventus kutwaa ubingwa wa Serie A mara nne,
akiifikisha pia katika fainali za Ulaya pamoja na
kuipeleka Ufaransa katika fainali za Euro 2016
ambapo walichapwa 1-0 na Ureno.
Mfaransa huyo atakuwa mchezaji wa nne
kusajiliwa na Man United dhini ya Mourinho
baada ya kuwanasa Eric Bailly kutoka Villarreal,
Zlatan Ibrahimovic aliyenaswa bure kutoka PSG
na Henrikh Mhkitaryan aliyechukuliwa kutoka
Borussia Dortmund.
Wakati dau la Pogba likianza kulalamikiwa na
wadau wengi wa soka kwamba haliendani na
kiwango chake, tayari nyota huyo ameanza
kupata watetezi akiwemo staa wa zamani wa
Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry
Henry.
“Sahau kuhusu Ufaransa, nadhani anaweza kuwa
mmoja kati ya viungo bora katika historia. Ana
ubora wa kufanya hivyo. Anahitaji kuwa makini tu
na kitu anachoweza kukifanya vizuri.” Alisema
Henry katika michuano ya Euro.
0 comments :
Post a Comment