Breaking News
Loading...

Advert

Friday, July 15, 2016

Breaking news#Maafisa 3 waJesh la polisi hapa nchini wamesimamiswa kazi.soma zaid.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira amewasimamisha kazi
watumishi watatu wa Jeshi la Polisi kwa
tuhuma za kufanya malipo hewa, yaani
kulipa posho ya chakula (Ration
Allowance) kwa watu ambao sio askari
Hatua hii ni mwendelezo wa uchunguzi wa
tuhuma za kufanya malipo hewa ya kiasi
cha sh. 305,820,000/= zilizopelekea
kusimamishwa kazi kwa Mhasibu Mkuu wa
Jeshi la Polisi Bw.Frank Charles Msaki wiki
iliyopita.
Kwa Mamlaka ya Katibu Mkuu chini ya
Kanuni ya 35(2)(b) ya Kanuni za Utumishi
wa Umma za mwaka 2003 zikisomwa
pamoja na Kanuni ya 37 ya Kanuni za
Utumishi wa Umma za mwaka 2003,
Kuanzia tarehe 13 Julai, 2016,
amewasimamisha kazi wafuatao: Bw.
Damian Aloys Bupamba ambaye ni
Mhasibu Daraja la II na Bi, Ida Dennis
Moyo Mhasibu Daraja la I kwa makosa ya
kufanya malipo ya posho ya chakula kwa
watu wasiostahili kwa kipindi cha kuanzia
mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.
Aidha kwa Mamlaka ya Katibu Mkuu chini
ya Kifungu cha 7(4) cha Sheria Na.8 ya
Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi na
Magereza ya Mwaka 1990 kama
ilivyorekebishwa na Sheria Na. 8 ya
mwaka 2015 kikisomwa pamoja na Kanuni
C.23(1)(b) ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi
la Polisi za mwaka 1995 zilizorekebishwa
mwaka 2013, kuanzia tarehe 13 Julai, 2016,
amemsimamisha kazi Mkaguzi Msaidizi
wa Jeshi la Polisi, Milambo Mwita Milambo
kwa makosa ya kufanya malipo ya posho
ya chakula kwa watu wasiostahili kwa
kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha
2013/2014 hadi 2015/2016.
Watumishi wote watatu wamehusika
kufanya malipo haya jambo ambalo ni
kinyume na Kanuni F.9 ya Kanuni za
Utumishi wa Jeshi la Polisi za mwaka 1995
kama zilizovyorekebishwa mwaka 2013.
Katibu Mkuu amewasimamisha wahusika
hawa ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma
dhidi yao unaofanyika kufuatia Uchunguzi
Maalamu wa Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi
la Polisi uliobaini makosa ya malipo hewa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.chanzo michuzi blog

0 comments :

Post a Comment

Back To Top