Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, July 30, 2016

CHADEMA kanda ya ziwa watangaza maandamano na kuyafungia Geita.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Kanda ya Ziwa kimetangaza
kufanya maandamano katika kanda hiyo huku
wakidai kuyafungia katika mji wa Chato ambao
ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Tamko la Chadema limetolewa na Katibu Mkuu
wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi,
Meshack Micus alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari jana ofisini kwake.
“Sisi kama Chadema kanda ya Ziwa hasa kanda ya
Victoria tayari tumeshawaelekeza wanachama
wetu wote, viongozi wetu wote na tayari mwitikio
ni mzuri. Na hadi leo tayari viongozi wetu wa
vitongoji 1973 wameshajiandaa wako tayari kwa
ajili ya kufanya maandamano na kufanya mikutano
ya hadhara katika maeneo yao,” alisema.
“Tutaandaa maandamano kutokea Kyelwa,
tutaelekea Misenyo, Bukoba vijijini na tutakuja
moja kwa moja mpaka Chato. Na wa Mwanza
tayari nimeshawaagiza kwamba maandamano yetu
tunaenda kuyafungia Chato,” aliongeza.
Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja baada ya
Rais John Magufuli kuwaonya Chadema
kutomjaribu kwa kufanya maandamano bila
kufuata utaratibu kwani hatawavumilia.
Rais Magufuli aliwataka wananchi kutokubali
kudanganyika na kufanya maandamano na
badala yake wajikite katika kufanya kazi
itakayowaletea maendeleo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
alitangaza kile walichokiita ‘Umoja wa
Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA)’,
akiwaalika wafuasi wake kufanya maandamano
nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top