Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, July 30, 2016

Wazir Jenista mhagama ametembela kiwanda cha ZFG wilayani mkuranga.soma zaid

Wafanyakazi wa viwanda wilayani
Mkuranga wamempongeza Mbunge wao
Abdalla Ulega kwa kufanikisha kumleta
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Jenista Mhagama kwa lengo la
kutembelea viwanda hivyo ili kujuwa kero
wanazokutananazo huku akiagiza
wanafanyakazi kupewa mikataba ya ajira
zao.
Waziri Jenista Mhagama ameagiza
halmashauri ya wilaya ya Mkuranga
kutengeneza sheria ndogo zitakazo kuwa
zinasimamia masuala mazima ya kazi
hususani viwandani na pia aliagiagiza
viwanda hivyo kuhakikisha wanaweka
awamu tatu za kuingia kazini ili kutoa
fursa kwa wafanyakazi hao kufanya kazi
kwa masaa nane kama sheria ya kazi
inavyoelekeza kinyume na hapo lazima
walipwe muda wa ziada kazini.
Jensta alitoa maagizo hayo leo wilayani
hapa baada ya kufanya ziara ya
kutembelea viwanda vya kuzalisha viatu
na ndala aina ya yeboyebo huku akikemea
vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa
na baadhi ya wamiliki wa viwanda
hivyo,ambapo ilidaiwa kuwa inafikia
hatua ya kuwataka kimapenzi wanawake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Jenista Mhagama akiwasili
katika kiwanda cha ZFG kilichopo wilaya
ya Mkuranga Kwa lengo la kusikiliza kero
za wafanyakazi wa viwanda hivyo leo
mkoani Pwani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Jenista Mhagama akizungumza
na wafanyakazi wa viwanda vya
kutengeneza viatu na ndala aina ya
yeboyebo kuhusu kukemea vikali vitendo
vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi
ya wamiliki wa viwanda hivyo leo mkoani
Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah
Ulega akizungumza na wafanyakazi wa
viwanda vya kutengeneza viatu na ndala
aina ya yeboyebo katika ziara ya
kutembelea viwanda hinyo mkoani Pwani,
kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Jenista Mhagama.
Wafanyakazi hivyo wakimsikiliza Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu),
Jenista Mhagama wakati alipofanya ziara

0 comments :

Post a Comment

Back To Top