Wema amekasirishwa na maneno ya mashabiki mitandaoni na kuwatolea makali .soma zaid
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu
ameonesha kuchoka na maneno mbalimbali
kutoka kwa watu hususani kwenye mitandao ya
kijamii kiasi cha kuamua kutoa yake ya moyoni
kwa watu wote ambao wamekuwa wakimfuatilia
maisha yake.
Wema Sepetu
Ameonesha kukasirishwa na baadhi ya
watuwanaomsema kwenye mitandao ya kijamii
hususani kuhusu mapungufu yake.
Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa
Instagram kuweka ujumbe mrefu kwa watu hao,
huku akiwataka wamuache aishi maisha yake
kwani hajawahi hata siku moja kwenda kuomba
msaada kwao, na kusema hata siku atakapokufa
atakufa mwenyewe na kama ni majibu kwa
Mungu atajibu mwenyewe.
“Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhari,
sijawahi hata siku moja kwenda kwa hata mmoja
wenu na kumgongea kuomba hata hela ya
chumvi. Maisha yangu yananihusu mimi na hata
siku nikifa nakufa mwenyewe, majibu kwa Mungu
naenda kujibu peke yangu. Niacheni jamani
nimechoka” aliandika Wema Sepetu
Mbali na hilo Wema Sepetu amewataka watu
ambao wanakereka na aina ya maisha ambayo
yeye anaishi waache kuyafuatilia kwani si lazima
kufuatilia kile akifanyacho au maisha anayoishi
yeye.
“Kama nakukera na maisha yangu basi
usiyafuatilie siyo lazima. Nisiheme sasa jamanii.
Naomba tafadhari kama mapungufu ni ya kwangu
mimi. Niacheni mimi nafanya kile kinachoridhisha
nafsi yangu maana sipendi kujikasirisha. Kwani
nikitajirika mimi au nikiwa masikini wewe
unapata faida gani. Jiulize kwanza hilo swali
ndiyo uanze kutoa maneno yako” alisema Wema
Sepetu
0 comments :
Post a Comment