Kiwanda cha kutengeza simenti Dangote kimetozwa faini ya sh.15ml.soma zaid
Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
( katikati) Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw.
Khatib Kizinga (kushoto) wakipata maelezo
toka kwa Bw. Sultani Pwaga wa kiwanda cha
Gas cha Madiba Mjini Mtwara wakati wa ziara
ya Naibu Waziri Mpina kiwandani hapo.
Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira NEMC limekitoza faini
ya shilingi milioni 15, kiwanda cha kutengeneza
simenti cha Dagonte Industry Limited kilichopo
mjini Mtwara, kwa kosa la kukiuka sheria ya
mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Katika siku ya pili ya ziara ya Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina mkoani Mtwara
imebainika kuwa kiwanda hicho cha Dangote
chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze kazi
ya kutengenza simenti, kimefanya uchafuzi wa
mazingira kwa kukosa sehemu maalum ya
kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na
utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na
makaa ya mawe kiwandani hapo.
Mkosa mengine ni kukosa vyoo kwa ajili ya
matumizi ya wateja wao ambao ni madereva na
makondakta wanao chukua mzigo wa simenti
kiwandani hapo, na kusafirisha kwenda sehemu
mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafisha
sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo
imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa
kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya
ya watumiaji wa eneo hilo.
Kwa Mujibu wa Naibu Waziri Mpina, adhabu hiyo
kwa kiwanda cha Dangote inayotakiwa kulipwa
ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na
urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo
pamoja na kuamsha uongozi wa kiwanda hicho
kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka
kiwanda hicho kuajiri afisa mazingira
atakayeshughulia changamoto hizo.
Kwa upande wake meneja utumishi na utawala
wa kiwanda hicho Bw. James Kajeli aliomba
serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda
kilikuwa kwenye mpango wa kufanya
marekebisho hayo na kuongeza kuwa
kutokufanya hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa
kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa baadhi ya
miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na
upatikani wa baadhi ya vibali kutoka katika
taasisi za serikali na si kudharau sheria ya
mazingira.
Naibu Waziri Mpina pia alitembelea kiwanda cha
kutengeneza gas cha Madiba na kukisifu kwa
utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa
viwanda vya serikali, kuwa mfano katika kutii
sheria za mazingira.
Ziara ya Mhe. Mpina pia ilihisisha ukaguzi wa
kiwanda cha kubangua korosho cha micro mix
cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha
Solvochemi pamoja na fukwe ya mnazi bay
iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko
ya tabia nchi.
Kushoto Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
akipata maelezo kuhusu uchimbaji wa malighafi ya
kutengeneza gypsum toka kwa bwana Hamisi Juma
meneja kiwanda cha Dangote
Eneo ya fukwe ya Mnazibay Mjini Mtwara
inavyooneka kuathirika na athari za mabadiliko ya
tabia nchi yaliyosababisha sunami mwaka 2015
february..Naibu Waziri Mpina Alitembelea eneo hilo
kujionea athari za mabadiliko ya tabia nchi.
0 comments :
Post a Comment