Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, July 30, 2016

Mapato hospital ya mhimbili yaongezeka hadi sh 4.8bilioni.soma zaid.

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) imefanikiwa kuongeza
mapato kutoka Sh 2.3 bilioni yaliyokuwa
yakikusanywa Desemba mwaka jana
hadi kufikia Sh 4.8 bilioni Mei mwaka
huu.
Hayo yamesemwa LEO na Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Profesa
Lawrence Museru wakati hafla ya
kutunuku vyeti kwa wafanyakazi bora
wa hospitali hiyo.
Hospitali hiyo imefanikiwa kuongeza
mapato kutokana na juhudi za
wafanyakazi ambao wanafanya kazi kwa
ari kubwa ili kutoa huduma bora kwa
wagonjwa.
Pia, wafanyakazi wamehamasika
kutokana na mkurugenzi huyo kuwajali
wafanyakazi na kusikiliza kero na
kuzitatua kwa wakati kwa mfano hivi
karibuni alilipa malimbikizo ya
wafanyakazi. Profesa Museru amesema
mapato hayo yameongezeka kutokana na
juhudi za wafanyakazi ambao
wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na
hivyo kusababisha mapato hayo kufikia
Sh 4.8 bilioni.
“Mafanikio haya yametokana na juhudi
za wafanyakazi. Mwaka jana niliwaomba
wafanyakazi wafanye kazi kwa bidii, na
wao walikubali. Imani yangu ni kwamba
posho kwa wafanyakazi wangu zitaanza
kulipwa baada ya bodi kupitisha ombi la
kuwaongezea. Nafikiri tukiwaeleza
vizuri bodi watatuelewa na hivyo
wafanyakazi watapata kile
tulichowaahidi,” amesema Profesa
Museru.
Mkurugenzi huyo amesema kwamba
hospitali imepata mafanikio makubwa
yakiwamo kuongeza huduma za afya
kwa mfano kuanzishwa kwa huduma ya
kusafisha figo, kuongeza wodi kwa
wagonjwa wanaohitaji uangali
maalumu, huduma za matumbo na
kuboreshwa kwa mazingira ya kutolea
huduma.
Amesema hospitali hiyo inajitahidi
kuongeza mapato zaidi ili iweze kulipia
huduma za umeme, huduma za simu,
ankra za maji pamoja na kudi za
majengo.
“Sisi hatufanyi biashara bali tunatoa
huduma kwa wagonjwa, tunapaswa
kuongeza mapato ili kulipia huduma
kutoka kwa washirika wetu akiwamo
Tanesco, kulipia maji na huduma za
simu,” amesema Kaimu Mkurugenzi
huyo.
Akizungumzia changamoto, Profesa
Museru amesema sehemu zinazotumika
kutoa huduma zinatakiwa kukarabatiwa.
Amesema miundombinu inapaswa
kukarabatiwa kwa kuwa imekuwa
ikichakaa kutokana na kuongezeka kwa
wagonjwa hospitali hapo.
“ Majengo ya hospitali hayajakarabatiwa
karibu miaka 20, hivyo tunapaswa
kukarabati sasa,” amesema.
Pia Profesa Museru amewapongeza
wafanyakazi bora ambao wametunukiwa
vyeti baada ya kuibuka kuwa
wafanyakazi bora.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence
Museru akizungumza katika hafla ya
kuwatunukia vyeti wafanyakazi bora 54.
Hafla hiyo imefanyika katika hospitali
hiyo.
Wafanyakazi wa hospitali hiyo
wakiwamo madaktari na wauguzi
wakimsikiliza Profesa Museru
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la
Muhimbili, Mziwanda Chimwege
akisoma risala kwa mgeni rasmi, Profesa
Museru katika hafla ya kuwakabidhi
vyeti wafanyakazi bora
Wafanyakazi wa hospitali hiyo
wakimsikiliza Mwenyekiti wa TUGHE,
Mziwanda Chimwege.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top