Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, July 10, 2016

Naibu spika Tulia Akson awakatisha tamaa ukawa.soma zaid.


Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson
amesema hoja ya wabunge wa Ukawa
kutaka aenguliwe kwenye wadhifa huo
inafanyiwa kazi na Kamati ya Haki, Maadili
na Madaraka ya Bunge ambayo iwapo
itaridhia, itarejeshwa bungeni kupigiwa
kura ambazo hata hivyo, hazitatosha kwa
uchache wao.
Dk Tulia alisema hayo jana wakati
akihojiwa na Tido Mhando katika kipindi
cha Funguka kinachorushwa na Azam TV.
“Hoja ikishakuja bungeni hapo sasa huwa
ni kampeni na baadaye kupigiwa kura.
Kwa kuwa waliopeleka hoja ni wabunge
wa upinzani, hivyo wanatakiwa kufikisha
idadi fulani ambayo kiuhalisia wao kwa
sasa hawana,” alisema.
Kwa karibu mwezi mzima kwenye Bunge
la Bajeti, wabunge wa Ukawa walimsusia
Dk Tulia na walikuwa wakitoka bungeni
kila alipoingia, tayari wameanzisha
mchakato wa kumuondoa madarakani kwa
madai kuwa hawatendei haki na anaminya
demokrasia ndani ya Bunge.
Dk Tulia alisema Katiba inatambua
kwamba kiongozi aliyechaguliwa anaweza
kuondolewa madarakani na wale
waliomchagua, hivyo wabunge wa
upinzani wametumia haki yao ya msingi
na kinachosubiriwa ni hoja yao kufanyiwa
kazi.
“Kanuni imeweka wazi na msingi ule
umejengwa kwenye Katiba kwa sababu
inatambua wale waliomchagua kiongozi
wasiporidhika naye wanaweza kumuondoa
madarakani. Nafarijika kuona wanachukua
hatua, hivyo mimi sina malumbano nao,”
alisema.
Hakuna maridhiano
Dk Tulia alisema hakuna maridhiano
yanayotakiwa baina yake na wabunge wa
Ukawa kwa kuwa hana malumbano nao,
bali kanuni na taratibu zinafuatwa
kufanikisha hoja yao ya kumuondoa
madarakani.
Naibu Spika huyo alisema maridhiano
huwapo baina ya watu wanaolumbana na
kwamba, baina yao hakutakuwa na suala
hilo.
Chanzo: Mpekuzi

0 comments :

Post a Comment

Back To Top