Watu 12 wamefariki dunia kutokana foleni nchini indonesia.soma zaid.
Wengi walikuwa wakisafiri baada ya
mwisho wa mfungo wa Ramadhan
Watu 12 wamefariki nchini Indonesia
kutokana na foleni ya magari
iliyosababisha mamilioni ya watu
kukwama barabarani siku kadha.
Wengi walifariki kutokana na kukosa maji
mwilini na uchovu. Watu wengi waliokuwa
wakisafiri kwa sherehe za kuadhimisha
mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan
walikusanyika katika makutano ya
barabara kisiwa cha Java.
Na hapo ndipo msongamano mkubwa wa
magari ulipotokea. Maafisa wa uchukuzi
nchini Indonesia wanasema vifo hivyo
vimetokea katika kipindi cha siku tatu.
Vyombo vya habari nchini Indonesia
vinasema wengi wa waliofariki ni wazee
ambao walikwama ndani ya magari chini
ya joto kali. Mtoto mmoja mchanga
alifariki kutokana na kinachodhaniwa
kuwa ni kupumua hewa chafu iliyojaa
moshi wa magari.
Chanzo: BBC
0 comments :
Post a Comment