Polisi wameua mutu mwingine mweusi kwa kumpigia risasi marekani.soma zaid.
Mtu mwengine mweusi amepigwa risasi na
kuuawa mapema leo na polisi wa trafiki katika
jimbo la Minnesota Marekani.
Dereva huyo ambaye alikuwa amembeba mpenzi
wake ndani ya gari lao alisimamishwa na polisi
katika eneo la Falcon Heights kisa , taa moja ya
upande wa nyuma wa gari lake ilikuwa
imepasuka.
Alipoulizwa leseni yake akanyosha mkonowe
kana kwamba anaichukuwa upande wa nyuma na
polisi huyo akampiga risasi 4 papo hapo.
Mpenziwe Lavisha Reynolds, na mwanawe
walikuwa naye ndani ya gari hilo.
Bi Lavisha Reynolds, alikuwa akipeperusha moja
kwa moja tukio hilo kupitia kwenye mtandao wa
Facebook.
Japo mkanda huo umefutwa kwenye Facebook
,watu wamejitolea kuuchapisha tena na tena.
Mkanda huo unamuonesha Philando Castile
akivuta pumzi yake ya mwisho huku afisa huo
akiwa amesimama wima kila mara akimtishia bi
Reynolds asidhubutu kusongeza mikono yake la
sivyo atampiga risasi.
Mwishowe bi Reynolds anakamatwa yeye na
mwanawe wanahamishwa hadi kituo cha polisi.
Video inaonyesha Philando Castile akifuja damu
ktoka kifuani huku polisi mwenye hasira akiwa
bado anamuelekezea Bunduki.
Bw Castile, 32, alikuwa msimamizi katika hoteli
moja inayowaandalia watoto wa shule ya
Montessori vyakula.
Mpenziwe anasema alikuwa na idhini ya kubeba
silaha halali.
Kisa hicho kinatokea huku kiandamana baada ya
mauwaji mengine ya mtu mweusi mjini Lousiana.
Mauaji ya Alton Sterling, yameibua hasira
miongoni mwa wenyeji wa mji huo wa Baton
Rouge ambapo Sterling alikuwa akiuza CD.chanzo bbc Swahili.
0 comments :
Post a Comment