Waasi 6000 wamekamatwa nchini Uturuki.soma zaid.
Utawala nchini Uturuki umevamia kambi za
kijeshi kote nchini kuwatafuta wanajeshi
wanaoshukiwa kuunga mkono mapinduzi ya
kijeshi yaliyozimwa siku ya Ijumaa.
Kambi za kijeshi zimevamiwa na kusakwa.
Katika oparesheni kwenye mji ulio magharibi wa
Denizli saa chacha zilizopita kamanda mmoja
wa kikosi cha jeshi na zaidi ya wanajeshi 50
walikamatwa.
Maelfu ya wanajeshi wamekamatwa.
Afisa mmoja wa ngazi ya juu serikalini
amesema kuwa jeshi limerejesha udhibiti katika
asilimia kubwa ya kambi za kijeshi japo kuna
baadhi ambazo zipochini ya usimamizi ya wale
walionga mkono mapinduzi.
Majaji takriban 3000 ambao wanatuhumiwa
kupinga serikali ya rais Reccep Teyyip Erdogan
wamesimamishwa kazi.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema
kuwa bunge litaamua ikiwa litabuni sheria ya
hukumu ya kifo.
Wale waliokamatwa wanatajwa kuwa wafuasi
wa kiongozi wa kidini raia wa Uturuki anayeishi
nchini Marekani Fethullah Gulen ambaye
analaumiwa kwa kupamnga mapinduzi hayo.
0 comments :
Post a Comment