Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 13, 2016

Wakurugenzi 5 wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi wasimamishwa kazi.soma zaid.

WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles
Tizeba amewasimamisha kazi wakurugenzi
watano wa idara tofauti katika wizara hiyo
kutokana na kuonesha udhaifu mbalimbali katika
utendaji wao na wengine kusababisha hasara
katika usalama wa chakula.
Waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Usalama wa Chakula nchini, Ombaeli
Lemweli kutokana na kutoa vibali vya ununuzi wa
mazao na kuuzwa nje ya nchi ilhali tathmini ikiwa
haijafanyika. Nafasi yake kuchukuliwa na Elimpaa
Kiranga aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Mazao
Mchanganyiko.
Aidha, ameagiza kusimamishwa kazi kwa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi
ya Chakula (NFRA), Charles Walwa na nafasi
yake kushikwa na Deusdedit Mpazi aliyekuwa
Meneja wa NFRA kanda ya Dodoma, kutokana na
kuharibu ghala la chakula na kusababisha hasara.
Viongozi wengine wa NFRA waliosimamishwa ni
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Huduma, Anna
Ngoo, Mkurugenzi wa Masoko, Mikalu Mapunda
na Meneja wa NFRA, Songea Jeremia Mtafya
ambao wametakiwa kupisha na uchunguzi
kufanyika mara moja dhidi yao.
Kadhalika, Dk Tizeba amemsimamisha kazi
aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Bahari Kuu, Rashid Hoza na nafasi yake
kushikwa na Hosea Mbilinyi aliyekuwa
Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi, lengo likiwa ni
kuimarisha ulinzi wa Bahari Kuu.
Mbali na nafasi hizo, pia Mkuu wa Kituo cha
Utafiti cha Uyole mkoani Mbeya, Dk Zakaria Maly
amevuliwa madaraka na kuhamishiwa katika
Kituo cha Utafiti Seliani mkoani Arusha
kuendelea na utafiti na badala yake nafasi yake
itachukuliwa na Arnold Msongi anayetoka Kituo
cha Utafiti Ilonga, Kilosa mkoani Morogoro.
Dk Tizeba alitoa maamuzi hayo jana Dar es
Salaam wakati akizungumzia masuala mbalimbali,
ikiwa ni mwezi mmoja baada yakuteuliwa na Rais
John Magufuli kushika wadhifa huo katika
mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri
yaliyompeleka aliyekuwa waziri wa wizara hiyo,
Mwigulu Nchemba kuongoza Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Waziri Tizeba alisema wakati ambapo tathmini ya
chakula nchini ikiwa haijakamilika, Kurugenzi ya
Usalama wa Chakula imekuwa ikitoa vibali vya
chakula kusafirishwa nje ya nchi, huku ikiwa
haijulikani kama chakula kilicho kinatosha au
hakitoshi na ili ziada ilindwe.
“Mbali ya kwamba hali ya chakula nchini ni nzuri
lakini kumekuwepo na wimbi la wafanyabiashara
wa ndani na nje ya nchi wakipewa vibali na
kununua mazao ndani ya nchi na kuyauza nje
ilhali tathmini ikiwa haijakamilika,” alisema
Tizeba.
Alitoa wiki mbili kuanzia sasa ukaguzi wa
chakula nchini uwe umefanyika ili kupatikana
kwa tathmini halisi katika kipindi cha mwaka
2015/2016 kwani ununuzi wa mazao hayo
umeonekana mkubwa na hali hiyo isipodhibitiwa
hali itakuwa mbaya zaidi.
Alisema vibali hivyo vimekuwa vikitolewa
kinyume cha utaratibu kwa kuwa tathimini
ilitakiwa kufanyika kwanza, hivyo Katibu Mkuu
amsimamishe kazi mkurugenzi huyo na
uchunguzi ufanyike dhidi yake pamoja na vibali
ambavyo vimekuwa vikitolewa tangu mwaka jana
kwani havina harufu nzuri.
“Hata hivi karibuni nimepata taarifa kuna
mfanyabiashara kapewa kibali cha kusafirisha
tani laki tatu kupeleka nchini Malawi, mfanye
uchunguzi wa vibali vyote alivyovitoa,” alisema
Tizeba.
Kuhusu NFRA, Dk Tizeba alisema umekuwepo
udhaifu mkubwa katika ghala la Songea, Dodoma
na Sumbawanga ambako mazao yameharibika na
kusababisha hasara huku uongozi wa wakala
licha ya kuombwa vibali vya kununuliwa kwa
mazao hayo kama chakula cha mifugo
havikutolewa.
Akizungumzia uvuvi bahari kuu, ameiagiza
Kurugenzi wa Uvuvi kubadilisha masharti ya
leseni ya uvuvi katika bahari kuu ili kuangalia
uwezekano wa kufanya ubia na wavuvi hao ili
Watanzania nao waweze kunufaika na mavuno ya
mazao hayo.
Alisema kwa wale ambao wana leseni
hazitofanyiwa mabadiliko lakini kwa zile mpya na
sheria haizuii kufanya hivyo.
Alisema hivi sasa zipo meli 105 zote zikitoka nje
ya nchi zikiwa zinaendelea na uvuvi na kuchota
chochote na kuondoka, huku mamlaka ya bahari
wakiwa wanayajua hayo, wakidai kuwa Tanzania
haina mahali pa kushushia.
Alisema kuanzia sasa meli zote ziambiwe mazao
yote watakayovuna ambayo ni tofauti na leseni
zao zinavyotaka yaletwe Dar es Salaam,
yagawiwe kama itakavyohitajika kwani Tanzania
imeendelea kuwa shamba la bibi kutokana na
kukosa uwezo wa kuvua katika bahari kuu.chanzo habar leo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top