Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 13, 2016

Wazir mkuu mpya wa uingereza ametangaza baraza la mawazir.soma zaid.

Pia amemteua Amber Rudd kuwa Waziri wa
Mambo ya Ndani, Michael Fallon ameteuliwa
kuwa Waziri wa Ulinzi.
London, Uingereza .. Ikiwa ni muda mfupi tu
kukabidhiwa funguo za ofisi zilizopo zilizopo
mtaa wa Downing nchini Uingereza Thereza May
amemteua Boris Johnson kuwa waziri wa Mambo
ya Nje pamoja na Philip Hammond kuwa Waziri
wa Fedha.
Pia amemteua Amber Rudd kuwa Waziri wa
Mambo ya Ndani, Michael Fallon ameteuliwa
kuwa Waziri wa Ulinzi.
Akizungumza baada ya kupokea ufunguo wa
makao rasmi ya waziri mkuu May amehakikishia
washirika wake na mataifa ya muungano wa
ulaya kuwa licha ya taifa hilo kuamua
kujiondoa,Uingereza inapania kujiunga na mataifa
shirika na kutekeleza wajibu wake katika
muungano wa mataifa huru duniani.
Amesema kuwa serikali yake haitanaswa na
mtego wa kuwasikiza mabwenyenye walio
wachache na kusahau wananchi wa kawaida.
Theresa May anakuwa waziri mkuu wa 13 kuwahi
kuiongoza Uingereza katika enzi ya Malkia
Elizabeth wa pili.
David Cameron amehutubia kwa mara ya mwisho
Bunge la Uingereza na kujibu maswali ya
wabunge.
Kisha kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa
Malkia Elizabeth wa Pili katika Kasri la
Buckingham.
Malkia amemtaka mrithi wa Cameron, May
kuunda Serikali ikiwa ni historia ya pekee kwa
Uingereza kupata kiongozi wa pili mwanamke
baada ya Magreth Thatcher.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) wameitaka
Serikali ya Uingereza kuharakisha mchakato wa
kujitoa rasmi katika umoja huo, lakini May
amedokeza kuwa hatauharakisha mpango huo
mashuhuri kwa jina la Brexit.
Changamoto kubwa inayomkabili ni pamoja na
kuizuia Scotland inayounga mkono Umoja wa
Ulaya dhidi ya kuitisha kura ya uhuru wake ili
kubakia katika EU na kuimarisha mahusiano
mapya ya kibiashara na kidiplomasia ili kujiandaa
kwa hali ya baadaye ya baada ya kujiondoa
katika umoja huo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top