Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, July 14, 2016

Maafisa 5 wa polisi wahofiwa kufariki nchini kenya baada ya kituo cha polisi kuvamiwa.soma zaid.

Maafisa kadha wa polisi wanahofiwa kufariki
baada ya mtu mwenye silaha kushambulia kituo
cha polisi eneo la Kapenguria, kaskazini
magharibi mwa Kenya.
Mtu huyo anadaiwa kuvamia kituo hicho
kumnusuru mshukiwa aliyekuwa amekamatwa
akishukiwa kuhusika katika ugaidi, gazeti la Daily
Nation limeripoti.
Gazeti hilo linasema huenda maafisa hadi watano
wameuawa.
Mkuu wa polisi wa kituo hicho Vitalis Ochido
anadaiwa kujeruhiwa.
Ufyatulianaji wa risasi bado unaendelea.
Tovuti ya habari ya Capital FM imemnukuu mkuu
wa polisi Joseph Boinnet akisema polisi zaidi
wametumwa eneo hilo.
“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anazuiliwa
alitwaa bunduki na kuanza kuvyatua risasi," Bw
Boinnet amenukuliwa. "Kituo hicho sasa
kimezingirwa na juhudi za kukabiliana naye
(mshambuliaji) zinaendelea."

0 comments :

Post a Comment

Back To Top