Kiwanda cha chuma cha mmi steel chatozwa faini ya sh.10ml jijini Dar es salaam.soma zaid.
Kiwanda cha kutengeneza vyuma cha MMI
Steel kilichopo katika eneo la viwanda
mikocheni jijini Dar es Salaam, kimetozwa
faini ya shilingi milioni kumi na kutakiwa
kulipa faini hiyo baada ya siku saba kwa
kosa la kukiuka sheria ya mazingira na
kanuni zake ya mwaka 2004, kwa
kutiririsha maji machafu katika maeneo
ya mtaa wa TPDC kwa warioba jijini dar
es salaa. Maji ambayo ni hatari kwa
mazingira na viumbe hai.
Adhabu hiyo imetolewa na Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
alipotembelea eneo la mtaa wa viwanda
mikocheni kufuatia uchafuzi wa mazingira
unaotokanao na utitiririshaji wa majitaka
katika maeneo hayo.
Wakati huohuo, Shirika la maji safi na
majita taka Jijini Dar es Salaam na Pwani
( Dawasco) limepewa siku kumi na saba
kumaliza tatizo la utiririshaji wa maji
taka katika mtaa wa TPDC mikocheni kwa
Warioba jijini Dar es Salaam.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu
Waziri Mpina Baada ya kufanya usafi
jumamosi ya mwisho wa mwezi wa tatu na
kutoa siku saba kwa DAWASCO na NEMC
kusimamia suala zima la usafi wa
mazingira na agizo lake kuupuzwa.
Awali, Mhe. Mpina alisema kuwa uchafuzi
wa mazingira hauwezi kuendelea
kuvumiliwa na lazima hatua za kisheria
zichukuliwe, na kuwaasa watendaji wa
taasisi za serikali kuyapa kipaumbele
maagizo yanayotolewa na viongozi wa
ngazi za juu za serikali kinyume na hapo
ni kutokutii mamlaka. “tasisi za serikali
lazima zifanye kazi kwa kushirikiana
kutokana na kwamba kumekuwa na
kutupiana mpira kati ya NEMC, dawasco
na Manispaa ya kinondoni katika suala
zima la utatuzi wa uchafuzi wa mazingira
katika mtaa wa TPDC.” Alisema.
Naibu waziri Mpina aliongeza kuwa
ifikapo tarehe 30/7/2016 asikutane tena na
tatizo la uchafu na harufu mbaya katika
mtaa wa TPDC kwani hali hiyo ni hatari
sana kwa afya ya wakazi wa maeneo hayo
na mazingira.
Kwa upande wake DAWASCO
ikiwakilishwa na Injinia Erick Jackson
alisema kuwa Tangu muheshimiwa Naibu
Waziri Mpina atoe agizo la uondoshwaji
wa majitaka na uboreshwaji wa
miundombinu katika mtaa huo, wamekuwa
wakifanya kazi na bado inaendelea na
kazi hiyo pamoja na kukabiliwa na
changamoto mbalimbali za kifedha na
ufundi.
Hata hivyo uongozi wa Halmashauri ya
wilaya ya kinondoni umelishitaki shirika
la maji safi na maji taka jijini dar es
salaam na Pwani DAWASCO ,kiwanda cha
MMI steel na Tembo Tiles kwa uchafusi wa
mazingira kwa kutirirsha maji taka.NA
EVELYN MKOKOI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga
Mpina akisikiliza maelezo kutoka kwa
mwenyekiti wa serikali za mtaa wa (TPDC)
Bw, Idrisa Hashimu kuhusu Uchafuzi wa
Mazingira Unaofanywa na viwanda katika
mtaa huo.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa
Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina akiwa katika ukaguzi wa Mazingira
katika kiwanda cha MMI steel
kinachotuhumiwa Kuchafua mazingira
katika mtaa wa TPDC.chanzo michuzi blog
0 comments :
Post a Comment