Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 24, 2016

Fuga kuku ujiongezee kipato.soma zaid

Pengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili
uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za
umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi
nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu
tena kwa uchache. Jambo hili anaweza
kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.Viko
vitabu vingi na tena siku hizi zinatolewa DVD za
jinsi ya kufanikiwa katika maisha. Utashangaa
mpaka unamaliza kusoma au kutazama DVD
hizo hujapata njia ya wazi sana sana utajilaumu
tu kwa kuendelea kupoteza fedha kwa
kuchangia miradi ya wajanja hao.
Wengine wanakuambia "amini tu kuwa wewe ni
tajiri na utafanikiwa" mh! INAWEZEKANA?
Afadhali hao, balaa zaidi ni wale ambao
wanayanadi mafanikikio na utajiri kwa mizizi,
hirizi na hata roho za binadamu wenzao!
Somo langu ni dogo lakini naamini wapo
watakaopata mafanikio makubwa sana. Sasas
kuwa makini zaidi. Unaweza kuanza kwa mtaji
wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo.
Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua
kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku
mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa
uwiano wa 1:4 . Hii ina maana kuwa
wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x
10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga
tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150
ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza
kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani
ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo
55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.
Ndugu mwanajamvi hayo niliyotoa ni makadirio
ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka
utakuwa na kuku zaidi ya 2000. Mwaka
utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya
kuuza kuku 1,000. Mwaka 2. 750(majike) x 10 =
7500 (uza wengine) 3000 x 10 = 30,000.
Kutegemea na uwezo wako mpaka mwisho wa
mwaka wa pili utakuwa umefanikiwa sana.
Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na
ufuatilie zaidi huku ukiacha kando uzushi wa
vitabu vya wasanii na DVD zao pia. NB.
Kumbuka kuku ninao wazungumzia hapa ni wale
wa kawaida sio wale mataahira (wa kisasa)
.Fuatilia zaidi kuhusu matibabu na matunzo
mengineyo..

0 comments :

Post a Comment

Back To Top