TPL kimeitaka serikal ya zanzibar imtenge maalimu seifu.soma zaid
CHAMA cha Tanzania Labour(TLP)
kimemuandikia barua Rais wa Mapinduzi wa
Zanzibar, Dk Mohamed Ali Shein na kumtaka
kuanzia sasa wamtenge Katibu Mkuu wa CUF ,
Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), kwa
kutomualika kwenye shughuli zozote za kitaifa
mpaka atakapojirekebisha na kuitambua rasmi
serikali iliyopo madarakani.
Aidha, kwa kuwa CUF inadai kwamba haiitambui
serikali hiyo basi ruzuku kwa chama hicho
isitishwe kuanzia sasa hadi hapo chama hicho
kitakapoitambua rasmi serikali hiyo na kuacha
kuhamasisha wananchi wasilipe kodi.
Katika barua ya chama hicho iliyosainiwa na
Mwenyekiti wake, Augustine Mrema ilisema
chama hicho kimesikitishwa na wanalaani
kitendo kilichofanywa Hamad ambaye pia
alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais kwenye
serikali ya Umoja wa kitaifa wa Zanzibar (SUK)
wakati wa maziko ya aliyekuwa Makamu wa
Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania na
Rais wa Zanzibar, marehemu Mzee Aboud
Jumbe cha kukataa kumpa Rais Shein mkono
wa kusalimiana.
Alisema kuleta tofauti za kisiasa msibani kwa
makusudi, Maalim Seif ameendelea kuwagawa
Wazanzibari kisiasa na kushindwa kumuenzi
marehemu Aboud Jumbe, ambaye pamoja na
kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu pia
ndiye aliyemlea Maalim Seif kisiasa.
Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu
wa marudio uliosusiwa na CUF, Maalim Seif
amekuwa akileta chokochoko na uchochezi
dhidi ya serikali ya Zanzibar akidai kwamba
haitambui na kuwataka wananchi wa Zanzibar
kugoma na kuwataka wasilipe ko
0 comments :
Post a Comment