Mahabusu ajinyonga jijini Arusha.soma zaid
Mahabusu aliyekuwa akishikiliwa katika kituo
kikuu cha polisi jijini Arusha aliyetambulika kwa
jina la Victoria Wenga (51) mkazi wa Lemara
jijini Arusha amejinyonga hadi kufa usiku wa
kuamkia jana kwa kutumia shuka lake bila
kuacha ujumbe wowote.
Marehemu alikamatwa Agosti 21 mwaka huu
majira ya Alfajiri kwa tuhuma za kuchoma moto
nyumba yake na maduka yake mawili kutokana
na ugomvi wa kifamilia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles
Mkumbo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika
Kituo cha Kikuu cha Polisi saa 6:20 usiku jana
wakati wenzake wakiwa wamelala.
“Polisi wa zamu alisikia kelele kutoka kwenye
chumba cha mahabusu wa kike ambapo polisi
walijitahidi kuokoa maisha ya mahabusu huyo,
lakini ilishindikanika,” alisema Kamanda
Mkumbo.
Mahabusu huyo, ambaye ni mkazi wa Lemara
jijini Arusha, alijinyonga kwa kutumia shuka lake
alilokuwa anatumia kujifunikia wakati yuko
mahabusi. Mtuhumiwa huyo, alijinyonga kabla
ya kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka
yake.
“Jana ilikuwa afikishwe mahakamani kujibu kosa
lililokuwa linamkabili,” alisema Kamanda
Mkumbo na kuwahakikishia kuwa hali ya
usalama kituoni hapo na tukio hilo, havihusiani
na sababu zozote za kiusalama.
Marehemu Victoria anadaiwa kuwa na ugomvi
wa kifamilia na mume wake aliyetambulika kwa
jina la Edward Wenga akimtuhumu kuzaa nje ya
ndoa kinyume na utaratibu.
Imeelezwa kuwa hicho ndo chanzo cha
marehemu kufikia hatua ya kuteketeza mali
walizochuma na mume wake ambazo ni maduka
mawili na nyumba ya kuishi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
chumba cha kuifadhia mahiti Hospitali ya Mount
Meru.
0 comments :
Post a Comment