Jipu limetumbuliwa#Bosi wa TPDC amesimamishwa kazi.soma zaid
BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo
ya Petroli Tanzania (TPDC) imemsimamisha
kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dk
James Mataragio.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya shirika hilo
na wadau mbalimbali wa masuala ya mafuta na
gesi, zimeeleza kuwa kusimamishwa kazi
kunatokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu (CAG) ya mwaka jana iliyoeleza kuwa,
TPDC ilikiuka taratibu za manunuzi ya umma
kwa kuipa upendeleo kampuni ya Marekani
kutafiti mafuta na gesi katika maeneo ya
kaskazini na magharibi mwa Ziwa Tanganyika,
Songosongo, Mandawa na Eyasi.
“Shirika kwa sasa si salama, kwani mkurugenzi
amepewa barua kutoka kwa mwenyekiti wa bodi
kusimamishwa kazi kuanzia jana (Jumatano)
kutokana na ripoti ya ukaguzi,” alisema mmoja
wa watoa taarifa.
Hata hivyo, mpaka jana jioni hakukuwa na
taarifa rasmi kuhusu kusimamishwa kazi kwa
mkurugenzi huyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Profesa Justin Ntalikwa alipoulizwa kuhusu
hatua hiyo, alisema anafahamu suala la
kusimamishwa kazi kwa Dk Mataragio, lakini
akaongeza kuwa, maelezo zaidi kuhusu
maamuzi hayo anayo Mwenyekiti wa Bodi ya
shirika hilo, Profesa Sufian Bukurura.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alipotafutwa kwa
simu kutoa taarifa rasmi za kusimamishwa kazi
kwa mkurugenzi huyo, hakupatikana kwani mara
zote simu yake ilisema inatumika.
0 comments :
Post a Comment