Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, August 25, 2016

Wizara ya Elimu kuhakiki vitabu vya la nne hadi la saba kujua ubor wake.soma zaid.

WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi imewaagiza wachapishaji wa
vitabu vya darasa la nne hadi la saba vyenye
Ithibati ya Vitabu na Vifaa vya Kielimu (EMAC),
kuvipeleka kwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)
, ili vitathminiwe kabla ya Septemba 30, mwaka
huu.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha wizara
hiyo ilisema kuwa Waraka Namba 4 wa mwaka
2014 umeipa TET mamlaka ya kufanya udhibiti
wa ubora wa vitabu na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia.
Taarifa hiyo ilisema, tathmini hiyo inafanywa ili
kuhakiki vitabu hivyo kwa kuwa mitaala
imeongezewa vitu vipya ambavyo inataka
kuhakikisha kuwa vimo katika vitabu hivyo au la.
Ilisema pia kuwa tathmini hiyo imelenga
kuvifanya vitabu hivyo viendane na wakati
uliopo kwa kuwa aina inayotumika kwa vitabu
hivyo ni tofauti na havifanani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vitabu vingine vina
kasoro ya kiuandishi, ndio maana wizara
imeagiza vihakikiwe upya.
Ilisema, “Ili kufanikisha zoezi hilo, nakala nne za
kila chapisho ziwasilishwe kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania kabla ya
Septemba 30, mwaka huu. Ilisema baada ya
muda huo, vitabu vitakavyokuwa havijafikishwa
kwenye taasisi hiyo kuhakikiwa vitafutwa
kwenye orodha ya vitabu vyenye ithibati.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top