Lowassa Mbowe watakiwa kuripoti polisi septemba mosi.soma zaid
Lowassa, Mbowe Watakiwa Kuripoti Polisi
Keshoi Septemba 1
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward
Lowassa na viongozi wengine waandamizi
wameitwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam kwenda kuripoti kesho Septemba
Mosi.
Hatua hiyo inatokana na viongozi hao kukamatwa
juzi, baada ya kufanya mkutano maalumu wa
ndani wa Kamati Kuu, na walipelekwa Kituo
Kikuu cha Polisi cha Kanda hiyo na kuhojiwa
kabla ya kuachiwa.
Mbali na Mbowe na Lowassa, viongozi wengine
wa Chadema waliokamatwa na kutakiwa kwenda
Polisi kesho ni Katibu Mkuu, Vincent Mashinji,
Naibu wake, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti
wa Chama hicho, Said Issa Mohammed.
“Wameitwa Polisi waende Septemba mosi kuripoti
baada ya jana kukamatwa na kuhojiwa
wakituhumiwa kukiuka maagizo ya Polisi,” alisema
Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene na
kufafanua:
“Lakini wanaweza kwenda au wakaanzia kwenye
maandamano kisha wakaenda Polisi kuripoti.”
Alisema maandamano hayo yatakuwapo kama
yalivyopangwa kwani maandalizi yake
yamekamilika.
Habari zaidi zilieleza, kwamba jana mchana
viongozi hao walikuwa wakifanya kikao Makao
Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam,
ambapo pia walikutana na wabunge wote wa
chama hicho kwa makundi tofauti.
Kwa mujibu wa mtoa habari ndani ya Chadema
makao makuu katika kikao hicho walijadili
mambo mengi ikiwa ni pamoja na suala la
utekelezaji wa Ukuta kesho.
Mmoja wa wabunge wa Chadema alisemai
kwamba walikuwa wakiwekana sawa kuhusu
maandamano yao.
Alibainisha kwamba katika mkutano huo ambao
Mbowe hakuwepo pia walijadili maombi ya
viongozi wa dini kuwataka kusitisha maandamano
hayo Septemba mosi.
“Viongozi wa dini wamekuwa wakituomba tusitishe
maandamano ya Ukuta Septemba mosi, tusubiri
hadi baada ya mkutano wa vyama vya siasa
Septemba tatu,” alisema Mbunge huyo wa Kanda
ya Ziwa.
Aliongeza: Katika mkutano huo, Lowassa na
viongozi wengine walijadili hayo na ikikubalika kwa
heshima ya viongozi wa dini maandamano ya Ukuta
yafanyike baada ya Septemba tatu.”
Hata hivyo, mwandishi alishuhudia wabunge
wengi wa chama hicho wakitoka katika mkutano
huo kimya kimya bila kutaka kuzungumza na
kabla muda uliopangwa kwisha, huku taarifa
zikieleza kwamba mkutano huo uliahirishwa
baada ya kuwepo taarifa za kutaka kuvamiwa na
Polisi.
“Tumeambiwa tusambaratike, tutajulishwa wapi
tutakutana tena, kama hapa au wapi,” alidokeza
mmoja wa wabunge hao.
Baada ya mkutano huo kuahirishwa, Lowassa
alitoka eneo hilo huku taarifa zikieleza alikuwa
akielekea kwenye moja ya hoteli jijini humo
kuungana na Mbowe ambapo walikuwa na
mazungumzo na baadhi ya viongozi wa dini.
0 comments :
Post a Comment