Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 31, 2016

Msanii Afande Sele anashikiliwa na Polosi mkoan Morogoro.soma zaid

Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro,
Afande Sele amedai anashikiliwa na jeshi la
polisi mkoani Morogoro kwa madai anagawa
pesa kwa watu ili kuwashawishi wajitokeze
katika maandamano ya UKUTA ambayo
yamepigwa marufuku.
Rapper huyo ambaye ni mwanasiasa na
aligombea ubunge kupitia cha ACT Wazalendo
katika uchaguzi uliyopita, amedai yupo mikononi
mwa polisi toka jana.
“Huku ni kushindwa kama sio kufeli, toka jana
nipo mikononi mwa polisi eti naambiwa
nimeratibu mkutano wa UKUTA , nimechapisha
T-shirt na kugawa fedha ili kesho watu
waandamane, pia kuaandaa mkutano maeneo ya
Msamvu.,” aliandika Afande Sele kupitia
facebook yake.
Aliongeza, “Nina zaidi ya mwezi sijakaa
maeeneo ya Msamvu zaidi ya kupita nikiwa
naelekea mikoani tena nikiwa kwenye gari
yangu. Ila hii aibu na fedheha kwa jeshi la polisi,
maamuzi ya kukurupuka . Tusubiri,”
Hata hivyo Bongo5 inaendelea kufuatilia taarifa
rasmi kutoka jeshi la polisi la Morogoro kuhusu
kukamatwa kwake.chanzo muungwana blog

0 comments :

Post a Comment

Back To Top