Chris Brown akamatwa na Polis Marekani.som zaid
Polisi mjini Los Angeles nchini Marekani
wanamshikilia saa wa muziki kutoka nchini
humo, Chris Brown kwa madai kutishia kumwua
mwanadada Baylee Curran kwa kumwekea
bunduki kichwani.
Polisi walifika katika nyumba ya Chris Brown
baada ya kupokea simu kutoka kwa Baylee
Curran kuwa Chris amemtishia bunduki kwa
kumwekea kichwani hivyo kufika katika nyumba
ya Chris Brown na kumkamata.
Taarifa zinasema kuwa, Chris alimwonyesha
mwanadada huyo bunduki baada ya kufika
nyumbani kwake akiwa na rafiki yake kwa ajili
ya kuzungumza mambo ya kibiashara na baadae
mwanadada huyo alionekana kuvutiwa na mtu
ambaye alikuwa amevalia cheni ya almasi
shingoni na baada ya Chris kugundua jambo hilo
alikasirika na kumwekea bunduki kichwani kisha
kumtaka aondoke.
Aidha inaelezwa kuwa Polisi wa LA kwa sasa
wanasubiri ruhusa ya mahakama ili kuwaruhusu
kuingia kufanya upekuzi kama ni kweli Chris
Brown ana bunduki katika nyumba yake ili hatua
zaidi zichukuliwa.
0 comments :
Post a Comment