Breaking News
Loading...

Advert

Monday, August 29, 2016

Tahadhari imetolewa kwa wakazi wa mikoa ambayo itashuhudia kupatwa kwa jua.soma zaid


Tahadhari imetolewa kwa wakazi wa mikoa
ambayo itashuhudia kupatwa kwa jua kuwa
kutazama jua moja kwa moja bila kutumia kifaa
chochote kunadaiwa kuwa na madhara kwa
mtazamaji kutokana na mionzi ya jua hilo.
Tukio la kupatwa kwa jua
Kupatwa kwa jua kunatarajiwa kutokea katika
mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ya Njombe
wilaya ya Wang'ing’ombe katika kijiji cha Litundu,
Mbeya wilayani Mbarali katika kijiji cha
Mpungarelini na mkoani Katavi ambako kupatwa
kwa jua kutaonekana vizuri kwa zaidi ya asilimia
97.
Tahadhari hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa
Njombe Dkt. Rehema Nchimbi wakati akiongea
na waandishi wa habari mkoani humo ikiwa
zimebaki siku chache kutokea kwa tukio hilo la
kihistoria.
Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa kuna
jitihada mbalimbali zinazofanywa na halmashauri
ya Waning'ombe kwa ajili ya kuweza kupata
vifaa mahususi kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo
bila kuacha madhara yoyote.
Tukio hilo la kupatwa kwa jua lilizinduliwa Julai
10 mwaka huu katika kijiji cha Litundu kwa mkoa
wa Njombe ambapo macho ya dunia nzima kitalii
yatatazama katika eneo hilo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top