Breaking News
Loading...

Advert

Monday, August 29, 2016

Waumini waingia kanisani na mabango kumpinga Askofu.soma zaid

Waumini waingia kanisani na mabango
kumpinga Askofu
Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki
wakiwa na mabango walipohudhuria ibada
kwenye Kanisa Kuu la Mtwara jana. Picha na
Haika Kimaro
Mtwara. Waumimi wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki,
Kanisa Kuu la Mtwara wameingia katika ibada
na mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali
wa kumpinga Askofu Mkuu wa dayosisi hiyo,
Lucas Mbedule kwa tuhuma za kukiuka katiba,
unyanyasaji wa watumishi na ubadhirifu wa
fedha za ushirika na dayosisi.
Hata hivyo, Askofu Mbedule amesema
asingependa kuyazungumzia suala hilo kwa
sababu walikaa kikao.
Umoja wa wazee ulitoa tamko ndani ya kanisa
hilo kutokana na tuhuma zinazomkabili askofu
huyo na kumtaka asijihusishe na mambo
yanayohusu usharika na dayosisi, ili kupisha
uchunguzi na kumwomba Mkuu wa KKKT, Dk
Fredrick Shoo kuunda tume kuchunguza tuhuma
hizo.
Akisoma tamko la wazee wa kanisa hilo, Amon
Mkocha amesema wanapinga uamuzi
uliofanywa na kikao cha halmashauri kuu
kilichofanyika mwezi huu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top