Naibu wazir TAMISEMI Seleman Jafo amemuagiza mkurugenzi kutatua mgogoro wa mradi wa soko la kahama.soma zaid
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo amefanya ziara ya Siku
mbili katika mikoa ya Shinyanga na Geita
na kukagua miradi mbalimbali.
Akiwa Mkoani Shinyanga, Jafo alitembelea
Hospitali ya Wilaya ya Kahama ambapo
alijionea changamoto mbali mbali ikiwepo
ya Jengo dogo linalotumiwa na kinamama
wakati wakujifungua kutokana na
hospitali hiyo kuzidiwa uwezo.
Kufuatia hali hiyo, Jafo amemuagiza
Injinia wa Wilaya kuhakikisha
wanaharakisha ujenzi wa Jengo kubwa la
kisasa la kinamama kwani fedha zipo za
Ujenzi huo ili wagonjwa wasiendelee
kupata mateso kwa michakato ya Ujenzi
mirefu isiyo na tija.
Kadhalika, akiwa wilayani Kahama, Naibu
Waziri Jafo ametembelea Mradi wa Soko
na kumuagiza Mkurugenzi wa Wilaya,
Andason Msumba, kuhakikisha anakaa na
timu yake ya Wataalamu ili kutatua
mgogoro wa Soko hilo kwa Maslahi
mapana ya wananchi wa Mji wa Kahama.
Amehitimisha Ziara yake mkoani
Shinyanga kwa kuzungumza na Watumishi
wa Halmashauri ya Mji wa Kahama na
Halmashauri ya Msalala ambapo
amewataka Watumishi kufanya kazi kwa
kujituma huku wakiepuka Uzembe
kazini,upendeleo, kupigana majungu, na
kuchukiana.
Mkurugenzi wa mji wa Kahama, Andason
Msumba akitoa maelezo kwa Naibu waziri
Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo
kuhusu mgogoro wa soko wanalolitaka
wananchi kutumika kwa maslahi ya
wananchi wa mji huo.
0 comments :
Post a Comment