Wazir Nape Nauye amevifungia kwa mda usiojulikana vituo vya radio Magic FM na Radio 5 kwa sababu ya uchochozi.soma zaid
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye ametangaza
kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo
vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya
Dar es Salaam kwa sababu za uchochezi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,
Waziri Nape amesema kuwa vituo hivyo
kwa nyakati tofauti zilitangaza habari
ambazo ndani yake zina uchochezi.
“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo
hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016)
hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,”
alisema Nape.
Aidha, amesema kuwa ameiagiza Kamati
ya Maudhui ya vyombo vya habari kuviita
vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha
kumshauri hatua zaidi ya kuchukua.
Waziri huyo ameeleza kuwa Serikali
inaendelea kutambua mchango mkubwa
wa vyombo vya habari katika kuleta amani
na ushirikiano nchini na sio vinginevyo.
Hivi karibuni, Nape alitahadharisha kuwa
vyombo vya habari vitakavyoripoti taarifa
ambazo ni za uchochezi vitakumbwa na
rungu la kuhusika kwa uchochezi pia.chanzo jamii forums
0 comments :
Post a Comment