Watumishi wa umma wameashwa kufahamu kanunu za utumishi.soma zaid
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angela Kairuki amewasisitiza
watumishi wa Umma kufahamu kanuni za
kudumu za utumishi wa umma ili
kutambua haki zao na kuepuka
kunyanyaswa na waajiri wao.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es
Salaam na Waziri huyo alipokuwa
akiongea na mwandishi wa habari kuhusu
utekelezaji wa mipango na mikakati
iliyowekwa na wizara yake katika kipindi
cha uongozi wa awamu ya tano.
Waziri Kairuki amesema kuwa ni muhimu
kwa watumishi wa Umma kufahamu kwa
undani maadili yaliyowekwa na Serikali
kwa ajili yao kwa kuwa yatawasaidia
kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu.
“Inawezekana maafisa utumishi walikuwa
wakizishikilia kanuni za utumishi wa
umma na kuona kama ni za kwao kana
kwamba mtu mwingine hatakiwi
kuzifahamu lakini napenda kutoa rai kwa
watumishi wote kuwa kanuni hizi ni za
kwetu wote hivyo ni muhimu kuzifahamu”,
alisema Mhe. Kairuki.
Mhe. Kairuki ameongeza kuwa kanuni za
utumishi za mwaka 1994 zilirekebishwa na
kwa sasa kanuni zinazotumika ni za
mwaka 2009 ambazo zinapatikana katika
tovuti za wizara mbalimbali hivyo
upatikanaji wake umerahisishwa tofauti
na zamani.
Pia amewataka watumishi kufuatilia
waraka mbalimbali wa maendeleo ya
kiutumishi inayotolewa na wizara hiyo
kwa kuwa itawasaidia kufahamu miundo
mipya ya utumishi inayotolewa, endapo
mtumishi hatofahamu mabadiliko hayo
atakosa taarifa muhimu.
Aidha, Waziri huyo amewakumbusha
Maafisa Utumishi kuwa kazi hiyo
wamesomea na watumishi ndiyo wadau
wao wakubwa hivyo kwa namna moja ama
nyingine kazi yao kubwa ni kuwasimamia
na kuwahudumia vyema watumishi hao
katika maeneo yao ya kazi.
“Napenda kutoa agizo kwa Maafisa
Utumishi wote kufanya kazi zenu kwa
umakini kulingana na kanuni za utumishi,
kwa kuwa kazi hiyo mmeisomea basi ni
lazima muwahudumie vizuri watumishi ili
nao waweze kupata ufanisi zaidi wa
kutekeleza majukumu yao”, alimalizia
Mhe. Kairuki.
0 comments :
Post a Comment