Benki ya Mkombozi imeendelea kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kutoa msaada wa Madawati Wilayani Bukoba.soma zaid
MKOMBOZI Commercial Bank ambayo ni
moja ya benki zinazokuwa kwa kasi
nchini, jana imekabidhi madawati mia
moja(100) kwa shule ya Msingi Ngarama
ikiwa ni katika juhudi za kuunga mkono
wito wa Mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli wa kuchangia madawati
mashuleni.
Madawati hayo yalikabidhiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bibi
Edwina A. Lupembe katika hafla
iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo
na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya
Bukoba Deodatus Kinawilo ambaye
alipokea rasmi madawati hayo.
Akikabidhi madawati hayo Mkurugenzi
wa banki hiyo Edwina Lupembe alisema
wao kama benki wameguswa na tatizo hili
la madawati na kuona ni jambo la busara
kuchangia ili watoto waweze kusoma bila
matatizo.
“Sisi Benki ya Biashara ya Mkombozi
tunathamini sana elimu na tunaunga
mkono jitihada mbalimbali za serikali za
kuboresha elimu hasa katika hili la
madawati ambapo hapo nyuma
tulishuhudia wanafunzi wengi wakikaa
chini. Wahenga walisema; Kama mpango
mkakati wako ni wa mwaka mmoja panda
mpunga kama mpango wako ni wa miaka
kumi panda miti lakini kama mpango
mkakati wako ni wa miaka 100 somesha
watoto. Wote tutakubaliana kuwa mpango
mkakati wa selikali yetu katika elimu ni
wa miaka 100.” alisema.
Alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa
uongozi wa shule hiyo kuhakikisha
madawati hayo yanatumiwa vizuri ili
wanafunzi wengi zaidi waweze kufaidi, na
kwa wanafunzi aliwataka wafanye bidii
katika masomo yao kwani sasa mazingira
ya kusomea yatakuwa bora zaidi na
kwamba elimu ni ufunguo wa maisha bora.
Bibi Lupembe alisema mbali na mchango
katika jamii, benki yake imekuwa katika
mstari wa mbele kuanzisha huduma
ambazo zinalenga kuwasaidia wananchi
hasa wenye kipato cha chini kama vile
huduma ya mikopo ya Mfuko wa Bima ya
Afya kwa wakopaji wa vikundi.
“Huduma hii ni endelevu na napenda
kutoa rai kwa wazazi na walimu waliopo
hapa wajiunge katika huduma ya mikopo
ya vikundi inayotolewa na Benki ya
Biashara ya Mkombozi kupitia tawi lake la
hapa Bukoba ambavyo vitawasaidia
kupata mikopo hii ya Mfuko wa Bima ya
Afya wa Taifa,alisema na kuongeza kuwa
hii italeta afueni kubwa kwani wanafunzi
pia wataweza kulipiwa kadi zao za
matibabu kupitia bima za wazazi wao
ambao watakuwa wamejiunga na vikundi
vya mikopo kutoka Benki ya Biashara ya
Mkombozi.
0 comments :
Post a Comment