Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, October 4, 2016

Rushwa ya mzungu imemtia hatiani polisi zanzibar.soma zaid

JESHI la Polisi visiwani Zanzibar, limesema
litamchukulia hatua za kinidhamu ofisa wake
mwenyewe cheo cha Sajenti ambaye alionekana
hivi karibuni akipokea rushwa kutoka kwa raia
wa kigeni.
Hatua hiyo, imekuja baada ya picha za video
kusambaa katika mitandao ya kijamii,
zinazomwonyesha askari huyo akipokea fedha
ambazo hadi sasa hazijajulikana kiwango chake
kutoka kwa raia huyo wa kigeni, ambaye
alikuwa na kosa la kutofunga mkanda.
Katika video hiyo, raia huyo anaokana kutoa
fedha na kumkabidhi askari huyo huku akiahidi
kumsaidia ili asikamatwe mbele ya safari.
Tukio hilo lilitokea eneo la Mkokotoni Mkoa wa
Kaskazini Unguja, ingawa askari huyo alitaja
eneo la Mahonda akionyesha nia ovu ya kutenda
kosa hilo bila kujijua kama anachukuliwa video.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani
Omar Makame alisema jeshi hilo linampongeza
raia huyo wa kigeni kwa kutoa taarifa hiyo.
“Jeshi la polisi linachukua nafasi hii kulaani
kosa hili, licha ya kua ni kosa la jinai
linalifedhehesha jeshi na kulitia doa kutokana na
dhamana kubwa lililokabidhiwa,” alisema.
Alisema kwa mujibu wa taratibu za jeshi hilo,
tayari limeanza uchunguzi mara moja na
kwamba litachukua hatua zinazostahili.
Kutokana na hali hiyo, Kamishina Hamdani
amewataka wamiliki wa makampuni ya simu za
mikononi kufufua mfumo wa upigaji simu
kutumia namba za dharura ambazo ni 111 na
112 ili kuwarahisishia wananchi kutoa taarifa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top