TCRA yakifungia kipindi cha Take one kinachorushwa na kituo cha Clouds media.
Dar es Salaam. Kamati ya Maudhui ya Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo
kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds
sambamba na kukifungia kwa kipindi kwa miezi
mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na
Kituo hicho.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Method
Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi
hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za
utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na
kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha
biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na
kutolinda maadili ya watoto.
“Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi
hicho kwa lengo la kupata njia bora ya
kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA
kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho
kufunguliwa,”alisema mapunda.
Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa
ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi
Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy
Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku
na kurudiwa kesho yake saa 7.00
0 comments :
Post a Comment