Rais wa Colombia asalimu amri akutana na viongozi wa upinzani ili kujadili jinsi ya kurejesha amani katika Taifa hilo.soma zaid
Rais wa Colombia,
Juan Manuel Santos
amekutana na
kiongozi wa upinzani
ili kujadili jinsi ya
kupata njia mbadala
ya kurejesha amani
katika taifa hilo.
Mkutano huu
unafanyika mara tu
baada ya wapiga kura
kupinga makubaliano
ya amani yaliyofikiwa
kati ya serikali na
waasi wa FARC.
Rais huyo aliteua afisa
mkuu kutoka
serikalini ili kujali njia
ambazo zitaweza
kuwasaidia kurejesha
historia ya
makubaliano ya amani
na kundi la FARC
ambalo limekuwa
katika mapambano
ndani ya taifa hilo
katika kipindi cha
nusu karne.
Rais wa zamani Alvaro
Uribe wa nchi hiyo,
ambaye aliongoza
kampeni ya kukataa
makubaliano hayo
hakuudhuria mkutano
huo na kuunda timu
yake mwenyewe.
Rais huyo wa zamani
anataka waasi
waliofanya uhalifu
kuchukuliwa hatua
kwa kuwekwa
gerezani na baadhi ya
viongozi wa FARC
kufungiwa kujihusisha
na kisiasa.
Nae kiongozi wa FARC,
Timochenko, anasema
ataendelea kuheshimu
makubaliano
yaliyofikiwa.
0 comments :
Post a Comment