Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, October 4, 2016

Papa amtuku Mtanzania tuzo ya heshima.soma zaid

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa
Francis amemtunuku tuzo ya heshima ya mfano
mwema Mtanzania, Janeth Mhella kutokana na
utumishi uliotukuka.
Mhella amekuwa Mwafrika wa kwanza
kutunukiwa tuzo hiyo na Papa Francis, kutokana
na kumtumikia vyema kiongozi huyo na kanisa
kupitia kazi aliyoifanya kwenye kituo cha redio.
Taarifa iliyotolewa jana, ilieleza tuzo hiyo ya juu
na ambayo mtu hawezi kuipata kwa urahisi
ilitolewa Alhamisi iliyopita na Kiongozi wa
Sekretarieti ya Mawasiliano ya Ofisi ya Papa,
Monsinyori Dario Vigno. Pia, watumishi wengine
watano walitunukiwa tuzo na sekretarieti hiyo.
Tuzo hiyo kwa Kiitaliano inaitwa ‘Pro Ecclesia et
Pontifice’ yaani medali ya Latini na kwa
Kiswahili fasaha ni medali ya kanisa na Papa.
Tuzo hiyo ya Kanisa Katoliki ilianzishwa na
Papa Leo wa 13 mwaka 1888.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top