Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, October 4, 2016

Watanzani wapewa somo ni lipi hilo .soma zaid

Naibu kiongozi mkuu wa waislam Shia
Ithnasharia Tanzania Sheikh Muhammad
Abdi akizngumza na wanahabari Leo Jijini
Dar es salaam PICHA NA EXAUD MTEI
Watanzania wametakiwa kuhakikisha
kuwa wanaishi katika njia za kumpendeza
mwenyezi mungu ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha maswala ya kuboresha hali
ya jamii yanayopewa kipaumbele,kukataa
kudhulumu,kuamrisha mema pamoja na
kukemea maovu kama mauaji ya
walemavu wa ngozi,matendo ya
kijambazi,ubakaji,ikiwa ni njia ya
kumuenzi Imam Hussein aliyekuwa mstari
wa mbele katika kukemea mambo hayo.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es
salaam na Naibu kiongozi mkuu wa
waislam Shia Ithnasharia Tanzania Sheikh
Muhammad Abdi alipokuwa anazungumza
na wanahabari kuhusu kuukaribisha
mwaka mpya wa kiislam mwaka ambao ni
wa 1438H katika kalenda ya kiislam
pamoja na kumbukumbu ya Imam Hussein
mkutano ambao umefanyika katika msikiti
wao uliopo Kigogo Post Jijini Dar es
salaam.
Kiongozi huyo amesema kuwa Imam
Hussein ambaye wanamkumbuka leo ni
moja kati ya viongozi wa dini ambao
aliwafunza watu namna ya kupinga
ukandamizaji,dhuluma katika jamii
pamoja na kutetea haki za wanyonge
hivyo ni wakati wa wananchi wa Tanzania
kuanza kufwata maneno yake na
kuhakikisha kuwa wanaenzi yale mema
aliyoyaacha katika jamii.
Amesema kuwa leo hii dunia inalazimika
kuitika wito wa Imam Hussein ili
kuinusuru dunia iliyotapakaa damu kila
kona,ambapo akitolea mfano wa
mashariki ya kati ambapo imekuwa
ikishughudiwa watoto wanavyochinjwa na
maelfu kukimbia makazi yao kwa sababu
ya uharibifu,huku pia katika bara la
Africa ikishughudiwa makundi ya kiigaidi
yakiibuka katika nchi nyingi ambapo
yamekuwa yakileta madhara makubwa
kwa wananchi wasio na hatia huku
akisema kuwa mambo haya ni mambo
ambayo yalikuwa yanamkera sana Imam
Hussein na kama angekuwepo angejitokeza
kupambana nayo.
Aidha Sheikh Muhammad Abdi
ameonyesha kuhuzunishwa na baadhi ya
matendo ambayo yamekuwa yakitokea
nchini Tanzania yakiashiria matendo ya
kigaidi na mauaji kwa wasio na hatia
ambapo ametoa wito kwa watanzania
kuacha mara moja maswala hayo na
kurudisha umoja na upendo miongozi mwa
jamii.
Aidha katika hatua nyingine kiongozi huyo
ametoa pole kwa watanzania wote
waliopatwa na janga la Tetemeko mapema
mwezi jana huku akitoa wito kwa
watanzania kuendelea kuwaombea na
kuwasaidia wahanga hao.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top