Dk .Didasi Masaburi meya wa zamani Dar amefariki dunia jana saa tatu na nusu usiku.soma zaid
Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk.
Didas Masaburi amefikwa na umauti jana majira
ya saa tatu na nusu usiku katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu
yake, Dk. Makongoro Mahanga ambaye alieleza
kuwa familia ipo katika taratibu za awali za
msiba huo na kwamba leo watatoa taarifa rasmi
na taratibu nyingine.
“Taarifa za kifo cha Dk. Masaburi ni za kweli
ingawa jioni hii sijaenda hospitali, ninafanya
mawasiliano na familia lakini taarifa kamili
kuhusu msiba zitakuwa zikitolewa na msemaji wa
familia ambaye tutamteua usiku huu, na kesho
(leo) tutaeleza kiundani,” Dk. Mahanga
anakaririwa na Mtanzania.
Marehemu pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la
Afrika Mashariki (EALA).
Dar24 inatoa pole kwa Taifa kwa ujumla kwa
msiba huu wa aliyekuwa kiongozi wa ngazi
mbalimbali akiutumikia umma. Apumzike kwa
Amani. Amina!
0 comments :
Post a Comment