Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, October 13, 2016

Kampuni ya Nyanza Road Works imepewa miezi minne kukamilisha ujenzibwa Barabara ya KM 50.som zaid

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa ameipa miezi minne
Kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works
kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya
Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50
kukamilika kwa wakati na wananchi wa Kibondo
na maeneo ya jirani kuweza kuitumia.
Waziri Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo wilayani
Kakonko mkoani Kigoma mara baada ya
kukagua barabara hiyo na kutoridhishwa na kasi
ya ujenzi wake.
“Mwezi wa pili mwakani nitarudi hapa kukagua
tena maendeleo ya ujenzi wa barabara hii
sababu bado kasi mnayokwenda nayo
hainiridhishi na kampuni hii ni ya kizalendo
ambayo ilitakiwa kuwa ya mfano”, amesema
Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amemsisitiza mkandarasi huyo
kuzingatia viwango bora vya ujenzi wa barabara
kama ilivyosainiwa kwenye mkataba na kumtaka
kuzingatia thamani ya fedha katika ujenzi
anaoufanya.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top