Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, October 22, 2016

Halmashauri ya jiji la Mwanza hupozeteza sh.1.3 bilion kila mwaka.soma zaid

HALMASHAURI ya jiji la Mwanza, hupoteza Sh.
1.3 bilioni kila mwaka kutokana na kodi ya
maduka zaidi ya 1024 inayokusanywa kuishia
katika mifuko ya baadhi ya wafanyabiashara
wajanja na watumishi wa jiji hilo, anaandika
Moses Mseti.
Kiomoni Kibamba, Mkurugenzi wa jiji la Mwanza
ameyasema hayo katika ziara ya kukagua
maduka ambayo hayajalipa kodi ya pango
mpaka sasa.
Kibamba amesema kuwa baada ya kufika katika
jiji hilo miezi miwili iliyopita na kuanza ukaguzi
wa miradi pamoja na kupitia mikataba
mbalimbali ikiwemo ya maduka hayo, amebaini
kuwepo udanganyifu unaoisababishia serikali
hasara kubwa.
Amesema kuwa hasara ya zaidi ya Sh. 1.3
bilioni imetokana na watendaji wa serikali katika
jiji hilo kujihusisha na vitendo vya rushwa na
ufisadi huku akitolea mfano maduka yaliopo
katika shule ya Sekondari ya Pamba tangu
mwaka 2006 yaliyoisababishia serikali hasara ya
Sh. 350 milioni.
“Ni kitu ambacho hakiingii kwenye akilini tangu
mwaka 2006 kampuni ya Lewico inapangisha
maduka ya serikali kwa gharama kubwa lakini
sisi tunachokipata hakiendani na
kinachopatikana.
“Mkataba wa maduka ya serikali unafanyika kati
ya shule na kampuni ya Lewico, suala hili
haliwezekani na kuanzia sasa hivi mikataba
yote itafanywa na halmashauri ya jiji,” amesema
Kibamba.
Kibamba amesema kuwa hayupo tayari kuona
watu wachache wakijinufaisha kupitia mali za
umma na kudai kwamba wote waliohusika katika
kuingizia serikali hasara watafikishwa katika
vyombo vya dola.
“Sijaja Mwanza kucheza nimekuja kufanya kazi,
wanaofanya udalali kwenye mali za serikali
waache mara moja na hizo kampuni zao hewa
sitaki kuziona katika jiji hili,” amesema
Kibamba.
Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara katika
eneo la Pamba, akiwemo Mashimba Kulwa
amesema wanamshangaa mkurugenzi huyo
kuwadai mikataba wakati wao waliingia na
kampuni ya Lewico.
“Sisi unatuonea bure kwa sababu mkataba wetu
tuliingia na kampuni ya Lewico ambayo ndiyo
inasimamia maduka yote, kama ni suala la
utaratibu kubadilika sisi tutaufuata lakini si
kutufungia maduka yetu,” amesema Mashimba.
Hata hivyo MwanaHALISI Online imeona
tangazo la tarehe 24 Septemba lililotolewa na
uongozi wa kampuni ya Lewico Limited,
likiwafahamisha wapangaji wake kuwa jiji la
Mwanza halina mamlaka yeyote ya kiutendaji
katika mikataba ya maduka hayo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top