Maalimu Seifu Sharifu Hamadi ahofia kukamatwa.soma zaid
Katibu Mkuu wa Chama Cha wananchi (CUF),
Maalim Seif Sharif Hamad amedai kuwa anaona
dalili za Serikali kumkamata na kumfungulia
mashtaka kutokana na harakati zake za
kuendelea kuipinga Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Akizungumza jana katika Msikiti wa Biziredi
visiwani humo wakati wa ibada ya Ijumaa,
Maalim Seif alidai kuwa anaona dalili za
kukamatwa na kushtakiwa Mkoani Dar es
Salaam, jambo alilodai ni mpango wa kufifisha
juhudi zake visiwani humo.
”Kuna dalili za kutaka kunikamata wanipeleke Da
es Salaam kama walivyofanya kwa masheikh,
lakini nasema yote hayo ni kupoteza muda wa
kuchelewesha haki ya Wazanzibari,” Maalim Seif
amekaririwa. ”Ieleweke kuwa haki hiyo haiwezi
kuzuilika tena kwa sasa,” aliongeza.
Maalim Seif ambaye amekuwa akidai alishinda
katika uchaguzi huo wa Oktoba 25 mwaka jana
na kupokonywa ushindi wake na chama chake
ambacho baadae kiliususia uchaguzi wa marudio.
Amekuwa akizunguka ughaibuni na tayari
amefikisha malalamiko yao kwenye Jumuiya ya
Kimataifa.
Katika hatua nyingine, mwanasiasa huyo
mkongwe na Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mstaafu,
alizungumzia madai ya Baraza la Mawaziri la
Mapinduzi ya Zanzibar kutaka kujadili
kuondolewa kwa mfumo wa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa (SUK) visiwani humo. Alisema kuwa
hakuna anayeweza kufuta SUK kwani ilianzishwa
kwa mujibu wa sheria baada ya wananchi kupiga
kura za maoni na maridhiano ya kisiasa.chanzo dewji blog
0 comments :
Post a Comment