Breaking News
Loading...

Advert

Monday, October 24, 2016

Kampuni ya Dangote imewafukuza kazi wafanyakazi 48.soma zaid

Mfumuko nchini Nigeria huenda umeathiri
kampuni ya Dangote Group inayomilikiwa na mtu
tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote.
Kampuni hiyo imeripotiwa kuwafuta kazi
wafanyikazi 48 wakiwemo wataalam 36 wa
kigeni na raia 12 wa Nigeria.
Ripoti zinasema kuwa hatua hiyo inatokana na
gharama ya juu ya kufanya biashara katika taifa
hilo na kampuni hiyo imeshindwa kupata fedha
za kigeni kuwalipa wafanyikazi hao wa kigeni.
Lakini msemaji wa Dangote Group Tony Chiejina
aliambia BBC kwamba ufutaji huo hauna
uhusiano na mfumuko.
Kampuni hiyo inasema kuwa ilikuwa inaimarisha
biashara zake na kwamba kazi zengine
zimechukuliwa na kampuni tanzu.
Kampuni ya Dangote Group ni miongoni mwa
kampuni zilizo na wafanyikazi wengi katika
sekta hiyo.
Miezi miwili iliopita ,kitengo cha habari cha
Bloomberg kiliripoti kwamba bwana Dangote
alipoteza dola bilioni 5.4 mwaka huu kutokana
na kuanguka kwa thamani ya sarafu ya Nigeria
,Naira.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top