Raia wanne wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa katika mji wa Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.soma zaid
Raia wanne wameuawa na wengine 14
kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea katika mji
wa Bangui ambapo mashirika ya kiraia nchini
Jamhuri ya Afrika ya Kati yalikua yalitoa wito wa
kusalia nyumbani kwa ajili ya kuomba kuondoka
kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya
Afrika ya Kati kinashtumiwa kushindwa kuyazima
au kuyadhibiti makundi ya watu wenye silaha.
"Askari wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya
Afrika ya Kati (Minusca) waliingilia kati mapema
Jumatatu hii katika mji wa Bangui ili kuondoa
vizuizi vilivyokua vimewekwa barabarani na
waandamanaji wanaowapinga," Minusca imebaini
katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu hii jioni.
"Minusca inalaani kabisa matukio ambayo
yaliathiri baadhi ya maeneo ya mji mkuu na
inasikitishwa kuona hali hiyo imesababisha vifo
vya raia wanne na kuwajeruhi wengine 14, ikiwa
ni pamoja na askari watano wa kikosi cha Umoja
wa Mataifa, " taarifa hiyo imeongeza. Vurugu hizi
"ni jaribio mpya la maadui wa amani kwa lengo la
kuvuruga kurejea kwa hali ya kawaida ya
kikatiba."
Minusca "pia inafutilia mbali kampeni ya
kupakwa matope dhidi askari wa Umoja wa
Mataifa wa kulinda amani na itaendelea na kazi
yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Minusca
pia inakumbusha kwamba vurugu zozote zile
dhidi ya askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda
amani zitapelekea wahusika kufunguliwa
mashtaka katika mahakama za kimataifa," taarifa
hiyo imehitimisha. RFI
0 comments :
Post a Comment