Wasomi wamezungumzi kuhusu uchanguzi Umeya Dar es salaamu.soma zaid
Dar es Salaam. Baada ya kuibuka malumbano
katika uchaguzi wa meya Manispaa za
Kinondoni na Ubungo baina ya CCM na vyama
vinavyounda Ukawa, wasomi wameshauri kanuni
zibadilike ili wanaochagua meya wawe madiwani
wa kuchaguliwa pekee.
Katika utaratibu wa sasa, mameya na wenyeviti
wa halmashauri huchaguliwa na madiwani,
madiwani wa viti maalumu, wabunge wa
majimbo wa kuchaguliwa, wabunge wa viti
maalumu na wabunge wa kuteuliwa.
Juzi, madiwani wa Chadema na CUF katika
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
walisusia uchaguzi wa meya kupinga wabunge
walioteuliwa na Rais John Magufuli kushiriki
kupiga kura, kwa kuwa walihamishwa kutoka
Manispaa za Ilala na Ubungo kuiwezesha CCM
ishinde umeya wa Kinondoni.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana amesema
utaratibu unaotumika sasa ndiyo unachelewesha
maendeleo ya wananchi kwa sababu viongozi
wanatumia muda mwingi kulumbana ili vyama
vyao vishinde.
Profesa wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Reuben
Niville amesema wananchi wanacheleweshewa
maendeleo kwa sababu ya malumbano ya kila
chama kutaka kuongoza halmashauri.
0 comments :
Post a Comment