Maofisa watatu wa Banki ya maendeleo (TIB) kizimbani kwa kupokea rushwa ya sh.5 mil.soma zaid
MAOFISA watatu wa Benki ya Maendeleo (TIB)
wamepandishwa kizimbani, wakikabiliwa na
mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh
milioni tano ili kumsaidia mteja apate hati ya
nyumba, iliyokuwa inashikiliwa na benki hiyo,
kama dhamana ya mkopo.
Washitakiwa hao ambao ni maofisa Ufilisi wa
benki hiyo, Edward Sizya, Aloyce Lufungulo na
Karani, Salum Salum, walifikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam. Walisomewa mashtaka manne na Wakili
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), Odessa Horombe mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.
Odessa alidai Oktoba mwaka huu katika ofisi za
TIB Tawi la Upanga, zilizopo Ilala, Dar es
Salaam, wakiwa maofisa Ufilisi wa benki hiyo na
karani waliomba hongo ya Sh milioni tano kwa
manufaa yao binafsi.
Ilidaiwa waliomba fedha hizo kutoka kwa
Gosbert Matale, kama kishawishi kumsaidia
Evelina Mdecha kukomboa hati ya nyumba
inayoshikiliwa na benki hiyo, kama dhamana ya
mkopo.
Wakili huyo alidai kuwa Septemba mwaka huu
katika ofisi hizo, Sizya akiwa mwajiriwa wa benki
hiyo aliomba Sh milioni tano kutoka kwa Evelina,
kama kishawishi kumsaidia kukomboa hati yake
ya nyumba inayoshikiliwa na benki hiyo na
inadaiwa Oktoba 12, mwaka huu, katika ofisi
hizo, Sizya alikubali kupokea Sh milioni mbili
kutoka kwa Evelina ili amsaidie kupata hati hiyo.
Katika mashtaka mengine, Sizya anadaiwa
Oktoba 18, mwaka huu, katika ofisi hizo kwa
manufaa yake alipokea Sh 200,000 kutoka kwa
Evelina, kama kishawishi cha kumsaidia
kukomboa hati hiyo. Washtakiwa walikana
mashitaka na Wakili Odessa alidai upelelezi
haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi
Novemba 8 mwaka huu itakapotajwa tena.
0 comments :
Post a Comment