Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, October 15, 2016

Mgogoro wa Ardhi umesababisha mama na wanae 2 kutembea kwa miguu siku 21 kwenda Dodoma kumuoa Wazir Mkuu.soma zaid

MKAZI wa Kilindi mkoani Tanga, Angela
Basso, akiwa na watoto wake wawili
Happy(7) na Janeth Peter(9), amelazimika
kutembea kwa miguu kwa siku 21 hadi
mkoani Dodoma kwa lengo la kumuona
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili amsaidie
kurudishiwa hekari 30 za mashamba yake
aliyozoporwa.
Basso alifika mjini Dodoma akiwa na
watoto wake hao, ambapo alisema aliona
ni vyema kwenda Dodoma kuonana na
Waziri Mkuu kutokana na kuporwa
mashamba na kuchomewa nyumba yake
katika kijiji cha Kwendigole wilayani
Kilindi na wanaume wawili ambao
waliojitokeza kwa nyakati tofauti wakidai
ni maeneo yao.
Alisema alipita hatua zote zinazotakiwa
kuomba mashamba, ambapo awali
alipatiwa hekari 10 na kijiji na
akazifanyia shughuli za kilimo na kujenga
nyumba yake ya kuishi, lakini baada ya
kwenda kujifungua alikuta mazao
yamefyekwa na yeye kutakiwa kuondoka
kwenye eneo hilo.
Mwanamke huyo alisema baada ya
kunyang’anywa alifikisha malalamiko
yake kuanzia uongozi wa kijiji hadi
wilayani na baadaye akapatiwa eneo
jingine la hekari 20, lakini alijitokeza mtu
mwingine na kudai eneo hilo ni mali ya
kanisa, licha ya kumiliki kihalali eneo la
Hembekali.
“Nilikwenda kushtaki kwa serikali ya kijiji,
kata na baadaye kwenda kwa mkuu wa
wilaya ambako iliamuliwa nirudishiwe
mashamba yangu, lakini hawakufanya
hivyo mwisho wa siku nikafukuzwa kabisa
kuishi kwenye eneo hilo,” alisema Basso
Mwanamke huyo alisema baada ya
kutimuliwa alianza kuishi maisha yake
kituo cha mabasi Muheza na baadaye
alifukuzwa kituoni hapo kwa madai watu
hawaruhusu kulala ama kuishi hapo na
ndipo akaamua kuanza safari ya Dodoma
baada ya kusikia Waziri Mkuu amehamia
Dodoma.
Akisimulia machungu ya safari yake,
Basso alisema akiwa njiani walikuwa
wakila mahindi ya kukaanga na maji ya
kunywa na kulala porini muda mwingine
giza linapowakuta katikati ya
pori.“Naomba kusaidiwa jamani nimeanza
kufuatilia tangu mwaka 2012 lakini bila
mafanikio jambo ambalo limechangia
familia yake kusambaratika kutokana na
kukosa pa kuishi huku watoto wangu hawa
wakikosa elimu kwa
kutangatanga,”alisema Mwanamke huyo
Basso aliomba Serikali itende haki ili yeye
aweze kupata haki yake ya kurejeshewa
mashamba yake na kurudi katika eneo
hilo ili watoto wake wawili wapate nafasi
ya kusoma. Mwanamke huyo alisema kwa
sasa amekuwa kama mkimbizi kutokana
na kukosa hana mahali pa kuishi huku
mumewe naye akiikimbia familia yake
baada ya kuporwa ardhi hiyo ambayo
ilikuwa kama kitega uchumi chao.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top