Msafara wa JPM wakumbana na foleni,mwenyewe ataka kutembea kwa miguu.soma zaid
Katika hali ambayo sio ya kawaida kwa kiongozi
kama rais wa nchi, Rais John Magufuli ambaye
yupo nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya
siku mbili amekutana na foleni wakati akielekea
katika eneo ambalo alizikwa Rais wa kwanza wa
Kenya, Jomo Kenyatta.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, aliuambia
mtandao wa Star wa Kenya kuwa Rais Magufuli
alikutana na foleni hiyo wakati akitokea katika
hoteli ya Intercontinental na kuelekea eneo la
alilozikwa Jomo Kenyatta na baada ya kuona
kuna foleni kubwa alitaka kutembea ili aweze
kufika eneo ambalo anataka kwenda kuliona.
Aidha baada ya kutoka eneo hilo alikuta tayari
maafisa wa usalama wameshaweka magari
mengine pembeni ya barabara ya Uhuru na hivyo
aliweza kupita kwa urahisi kuelekea ikulu
kukutana na mwenyeji wake, Rais Uhuru
Kenyatta.
Baada ya kuwasili ikulu JPM alionana na Rais
Kenyatta na kufanya mazungumzo kisha
kulihutubia taifa la Kenya kuhusu mahusiano ya
Kenya na Tanzania na mipango ambayo
wameiweka baada ya kufanya mazungumzo.chanzo dewji blog
0 comments :
Post a Comment