Rais Obama amesema Trumpu hafai kuwa rais wa Marekani.soma zaid
Rais wa Marekani Barak Obama amewataka
wanasiasa wa Republican kujiondoa rasmi
kumuunga mkono Donald Trump kama mgombea
wao,kwa madai kuwa hafai.
Katika mkutano wa hadhara na wafuasi wa
Hillary Clinton, Obama amesema kuwa haina
maana kukemea hotuba tata ya Trump kuhusu
wanawake, huku wakiendelea kumuunga mkono
katika nafasi ya Urais, na kudai kuwa hiyo haina
maana kwake.
Viongozi wakubwa wa Republican akiwemo
msemaji wa chama hicho, Paul Ryan
wamejiweka mbali na Donald Trump baada ya
kuwekwa hadharani video inayomuonesha Trump
akiwakashifu wanawake.Hatua hiyo imekuja huku
asilimia 10 ya viongozi wa chama cha
Republican wakimtaka Trump kujiondoa katika
kinyang'anyiro hicho .
Trump alimjibu Ryan,kuwa kwa matammshi hayo
ameonyesha kuwa yeye ni kiongozi dhaifu
,amesisitiza kwamba amejipanga kuipigania
Marekani kwa njia anayoona inafaa.
0 comments :
Post a Comment