Breaking News
Loading...

Advert

Monday, October 10, 2016

Stephen Wasira ameendelea kupinga ushindi wa Ester Bulaya mahakamani.soma zaid

Shahidi wa tatu katika kesi namba moja ya
mwaka 2015 ya kupinga matokeo ya ubunge wa
jimbo la Bunda Mjini, Stephen Wasira leo
amepanda katika kizimba cha mahakama kuu
kanda ya Mwanza, inayoketi mjini Musoma kutoa
utetezi wake, huku ulinzi mkali wa askari polisi
wenye silaha za moto, mabomu ya machozi na
mbwa ukiwa umeimarishwa.
Wasira ambaye alitumia muda wa saa 2 na
dakika 26 kutoa ushahidi wake huku akihojiwa na
wakili wa mlalamikiwa wa kwanza Ester Bulaya,
ameiambia mahakama kuu chini ya jaji Noel
Chocha kwamba uchaguzi katika jimbo la Bunda
mjini ulikuwa haramu kutokana na kugubikwa na
ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni
kulikofanywa na msimamizi wa uchaguzi kufuatia
kuwepo kwa ongezeko la vituo vya kupigia kura
kutoka 190 hadi 199, sambamba na ongezeko la
idadi ya wapiga kura kutoka watu 69,369 hadi
164, 794 bila taarifa yoyote.
Mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye aliangushwa
na mgombea wa chama cha demokrasia na
maendeleo ( CHADEMA ), katika uchaguzi mkuu
uliopita kwa kura 19,000 dhidi ya 28,568
alizopata mshindi Ester Bulaya, amemlalamikia
msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bunda mjini
kuongeza vituo 9 kwenye kata za kabasa, Bunda
mjini, Bunda stoo, Manyamanyama,
Nyamakokoto, Wariku na Guta pamoja na
kuhamisha kituo cha Mchalo na kukipeleka
mahali kusikojulikana bila kuvishirikisha vyama
vitano vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi huo.
Mapema wakili Tundu Lissu, baada ya kupitia
kiapo cha shahidi huyo Stephen Wasira aliiomba
mahakama hiyo kuondoa aya ya 3b, kirumi i (ii),
( iii ) na ( iv ) pamoja na 3c, ambazo
zingewezakuleta mambo mapya katika shauri hilo
kinyume na masharti ya 23 ya kanuni za
uendeshaji wa uchaguzi za mwaka 2013 kama
zilivyofanyiwa marekebisho, hoja ambayo
ilikubaliwa na jaji Noel Chocha.
Mara kwa mara jaji chocha alilazimika kuingilia
kati kwa kumtaka wasira kujibu maswali ya wakili
Tundu Lissu, huku Wasira akionekana dhahiri
kuwa na majibu ya kujiamini; ambayo wakati
mwingine yaliwafanya wasikilizaji kuangua
kicheko hasa pale alipodai kuwa hamfahamu
katibu mkuu wa Chadema Dk. Vincent Mashinji
zaidi ya Dk. Wilbroad Slaa, ili kujiridhisha iwapo
Ester Bulaya aliwahi kujaza fomu ya bajeti za
gharama za uchaguzi ambayo kisheria hupelekwa
kwa msajili wa vyama vya siasa mwenye uwezo
wa kumwekea pingamizi mgombea aliyekiuka
utaratibu.
Kipindi cha mchana kilianza kwa mawakili
Costantine Mutalemwa, Yasin Memba na Hajra
Mungula wanaowatetea wapiga kura wanne wa
jimbo la Bunda mjini waliofungua kesi hiyo
mahakama kuu kanda ya Mwanza kumhoji shahidi
huyo wa tatu Stephen Wasira baada ya wakili
Tundu Lissu kuhitimisha maswali yake.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top