Breaking News
Loading...

Advert

Monday, October 10, 2016

Mfanyabiashara anayedaiwa kusema serikali iko mfukoni mwake kuchunguzwa.

DC Hapi aamuru kuchunguzwa
mfanyabiashara anayedaiwa kusema
‘serikali iko mfukoni mwake’
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Salum
Hapileo asubuhi amewatembelea wananchi wa
Tegeta kwa ndevu eneo ambalo baadhi ya
wananchi walionekana kwenye vyombo vya
habari wakilalamika kuhusu kufanyiwa hila na
mfanyabiashara mmoja ajulikanae kwa jina la
Emily Reshea aliyechimba shimo mbele ya
nyumba za watu na kuziba njia za wananchi
kupita kama mbinu ya kuwalazimisha wamuuzie
maeneo yao.
Hapi akiwa katika eneo hilo akiambatana na
wataalamu wa mipango miji, mhandisi wa
manispaa na askari wa jeshi la polisi ameagiza
kuvunjwa kwa ukuta ulioziba njia za wananchi
kupita, kufukiwa kwa shimo lililochimbwa kabla
ya saa 12 jioni leo october 10 2016 na kumtaka
OCD Kawe kuchunguza tuhuma za
mfanyabiashara huyo kudaiwa kusema kuwa
“serikali iko mfukoni mwake” na ikibainika kuwa
ni kweli akamatwe mara moja na kuhojiwa na
vyombo vya dola.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top