Tanzania na Umoja wa Maifa(UN) kuimarisha ulinzi amani katika mataifa mbalimbali.soma zaid
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika
mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga
amesema ushirikiano wa Tanzania na umoja wa
mataifa (UN) wataendeleza ulinzi wa amani
katika mataifa mbalimbali kama wanavofanya
kwa Sudan ya kusini.
Akizungumza katika hafla ya miaka 71 ya umoja
huo Dar es salaam , Balozi Mahiga amewataka
Vijana nchini kuchangamkie fursa za ajira
zinazopatikana umoja huo.hafla za miaka 71 za
umoja wa mataifa zimehudhuliwa na viongozi
mbalimbali wa kitaifa na kimataifa huku suala la
ulinzi ' pamoja na amani likiwa limepewa
kipaumbele kwa mataifa
Naye Mwakilishi wa Mashirika wa Umoja wa
Mataifa Alvaro Rodriguez amezitaja changamoto
zinazoikabili UN ni ongezeko la vijana ambapo
wengi huwa wanashindwa kuendana na
ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia kutokana na
miundombinu ya Elimu kutokuwa Rafiki.
Rodriguez ameongeza kuwa Ili kuhakikisha UN
inakabiliana na Changamoto hiyo wameweka
nguvu zaidi katika kuboresha Miundombinu ya
Elimu barani Afrika ili vijana kuweza kuendana na
kasi ya utandawazi ili kuweza kujiajiri. Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,Balozi Augustine Mahiga akizungumza
kwenye hafla ya miaka 71 ya umoja wa mataifa
(UN) jana jinini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza
kwenye hafla ya miaka 71 ya umoja mataifa
(UN) jana jinini Dar es Salaam. (P.T)
Chanzo mjengwa.
0 comments :
Post a Comment