Vigogo watatu wakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya sh.8 bilion.soma zaid
Vigogo watatu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA) wakabiliwa na kesi ya
kuomba rushwa ya dola za Marekani milioni nne
sawa na zaidi ya shilingi bilioni nane za
Tanzania.
Hayo yamesemwa na Wakili Mkuu wa Serikali ,
Mutalemwa Kishenyi akiwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaaamna. Na
kuwataja vigogo hao ni aliyekuwa Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA,
Epharaim Mgawe, Mkurugenzi wa Uhandisi TPA,
Bakari Kilo, Meneja Manunuzi TPA Theophil
Kimaro, na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya DB
Shapriya Ltd Kishor Shapriya.
Aidha, Wakili Kishenyi amesema washtakiwa hao
wadaiwa kati ya mwaka 2009 na 2012 mahali
pasipojulikana wakiwa katika nyadhifa zao kupitia
Wakala wa Kampuni ya DB shapriya Ltd
waliomba rushwa ya dola za Marekani milioni nne
kama kishawishi cha kuiwezesha kampuni hiyo
kushinda zabuni yenye namba
AE/0116/2008-2009/10/59 kwa ajili ya ujenzi wa
bomba la mafuta TPA katika RAS ya Mji Mwema.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa
walikana kuhusika na kutenda makosa hayo.
Wakili Kishenyi alisema upelelezi wa kesi bado
unaendelea, pia hawana pingamizi la dhamana
endapo washtakiwa watatimiza masharti ya
dhamana yatakayotolewa na mahakama.
Vigogo hao waliachiwa kwa dhamana baada ya
kutimiza masharti ya dhamana yaliyowataka
kuwa na wadhamini wawili waaminifu
watakaosaini hati ya dhamana ya Sh milioni 500
kwa kila mmoja.
0 comments :
Post a Comment